TAASISI ya Kiislamu ya Islamic Peace Foundation (IPF) kwa kushirikiana na Baraza la Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI), zimesema Chadema si chama cha kidini. Tamko hilo walilitoa jana kwa vyombo vya habari na kudai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na dhana waliodai imeenezwa katika jamii ya Watanzania na Waislamu nchini kuwa Chadema ni chama cha kidini. “Tunatoa mwito kwa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuipuuza dhana hii na kuwapuuza wale wanaoieneza ili tuwaunge mkono watu wote wanaotetea maslahi ya wanyonge na rasilimali za taifa letu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa IPF, Shehe Sadik Godigodi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi wa taasisi hizo baada ya kutafakari dhana hiyo na hatima ya Taifa, wamebaini kuwa hakuna ukweli wowote wa jambo hilo bali ni propaganda. Taarifa hiyo pia imewataka Watanzania kupuuza propaganda hiyo kwa kile ilichodai kuwa haikuanzia Chadema, bali katika Chama cha Wananchi (CUF). Shehe Godigodi alidai kuwa CUF ilidaiwa ni ya kikabila na kidini (Uislamu) na kuleta athari kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000. “Hali kama hiyo sasa tunaiona inajitokeza ndani ya Chadema ambacho mwanzo kiliitwa cha kikabila kwa maana ya chama cha Wachaga. “Lakini baada ya chama hicho kuimarika katika uchaguzi wa mwaka 2010 kama ilivyokuwa kwa CUF, kikabadilishiwa wimbo na kuwa chama cha udini yaani Ukristo,” ilieleza taarifa hiyo. Viongozi wa taasisi hizo katika taarifa yao hiyo wamedai kuwa udini ndani ya Chadema haupo kwa kuwa chama hicho kama vilivyo vyama vingine kina Waislamu, Wakristo na wasio na dini. Waliwataka Waislamu kutowabagua wenzao walio katika chama hicho kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha matakwa ya dini ya Kiislamu. | ||||||||
PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.
Wednesday, 26 October 2011
TAASISI ZA KIISLAMU ZAISAFISHA CHADEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment