PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Saturday, 25 February 2012


Kabla ya kubadilishwa jina


Mambo ya sabasaba...wadau kwa raha zao


Mnapakumbuka hapo wadau?

Friday, 24 February 2012


Tembo akijivinjari pembeni ya mount kilimanjaro in Tanzania


Twiga mpenda amani..hapo akimuokoa zebra
alietaka kuliwa na simba


Kitu kamili ndani ya bongo..kwenye goz goz anapaa

Sunday, 12 February 2012

PICHA OF THE DAY


The Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja and the visiting U S Assistant Secretary of State for African Affairs Johnnie Carson, display a joint statement of Principles of the Partnership for Growth, shortly after they signed the agreement at the Prime Minister’s Office in Dar es Salaam yesterday. Left is the U S Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Leinhadrt. Tanzania is one of four countries selected for Partnership for Growth (PfG) Initiative.

NOTI MPYA ZA MANDELA


Nelson Mandela
Afrika Kusini inatoa noti mpya zenye picha ya Nelson Mandela.
Rais Jacob Zuma alitangaza hayo mjini Johannesburg katika kutimiza miaka 22 tangu Bwana Mandela kuachiliwa huru baada ya kifungo kirefu.
Alisema kufunguliwa kwa Bwana Mandela ndio ulikuwa mwanzo wa awamu mpya ya matumaini nchini Afrika Kusini.

UMOJA WA MATAIFA WAOMBWA USAIDIE SYRIA


Nabil El-Araby, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu
Jumuia ya nchi za Kiarabu imeamua kuuomba Umoja wa Mataifa uisaidie kuunda ujumbe wa amani wa pamoja, kuutuma Syria, ili kumaliza ghasia nchini humo.
Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa jumuia hiyo, unaofanywa Cairo.
Piya mawaziri walikubali kusitisha uhusiano wa kibalozi na Syria, na kuanza mazungumzo na upinzani wa Syria.
Mkuu wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu, Nabil El-Araby, aliuambia mkutano kwamba wakati umefika kuchukua hatua thabiti kumaliza adhabu za watu wa Syria.

ZAMBIA MABINGWA AFRICA 2012


Zambia
Zambia yawaangusha Tembo
Zambia imechukua ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 baada ya kuwafunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 7-8.
Mchezo huo ulimaliza dakika 90 za kawaida, kabla ya kwenda muda wa ziada, na hadi katika mikwaju ya penati.
Awali nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba alikosa penati ambayo ingeipa ushindi kabla ya kumalizika kwa dakika 90 za kawaida.
Ivory Coast wamekosa penati 2 kati ya walizopiga ambapo Kolo Toure na Gervinho walikosa mikwaju hiyo.

Monday, 6 February 2012

DUNIANI KUNA MAMBO JAMANI!!!


WEZI WAISHIO JELA

Jela
Jamaa wakiiba wanarudi ndani
Polisi na maafisa nchini Australia wanafanya uchunguzi kuhusu madai kuwa wafungwa wawili wanatoroka gerezani na kuingia mitaani kufanya uhalifu na kisha kurejea tena gerezani kimya kimya.
Uchunguzi huo umeanzishwa baada ya watu wawili wakiwa wamevaa sare za magereza kuingia katika duka moja karibu na mji wa Bathurst na kuiba kiasi kidogo cha fedha.
Gari la rangi nyeupe aina ya Toyota HiLux 4x4 ambalo walionekana wakiendesha wezi hao lilikutwa limetelekezwa saa kadhaa baadaye karibu na gereza la Oberon.
Gari hilo lilikuwa limeibiwa mapema mwezi uliopita, na hivyo kuzua hofu kuwa wezi hao wana tabia ya kutoroka na kurejea gerezani.
Mkulima mmoja naye amesema alikuta nyumba yake imevunjwa na vitu kuibiwa. Mtandao wa couriermail.com umesema polisi wametoa taarifa ikisema uchunguzi unafanyika kuhusiana na matukio hayo, na kuona kama wataendelea au hawataendelea.

UKAME WAATHIRI HADI BANGI

Mvua
Ukosefu wa mvua umesababisha ukame
Hali ya ukame imekumba eneo la kaskazini mwa Mexico kiasi kwamba imeathiri hadi kilimo haramu cha bangi na opium poppies zinazotumika kutengenezea dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa kamanda wa kijeshi wa Mexico, Jenerali Pedro Gurrola ukosefu wa mvua umesababisha kilimo cha bangi kudorora kwa kiasi kikubwa.
Gurrola amesema uchunguzi wao umegundua mashamba machache ikilinganishwa na miaka iliyopita. "Huwa tunaona bangi nyingi" kamanda huyo amewaambia waandishi wa habari "kama mnavyoona hali ni kavu sana" amesema kamanda Gurrola.
Hata hivyo amesema wakulima hao wanatafuta mbinu nyingine kama vile kupanda karibu na mito au kufanya kilimo cha umwagiliaji maji kwa kutumia pampu.

SHULE ZA KUSOMA NYOTA

Mkono
Nani kaona... watoto wanasomwa viganja
Shule kadhaa za chekechea nchini Uchina zinatoza wazazi karibu dola mia mbili ili kusoma viganja vya watoto na kubashiri kama watoto hao watakuwa na mafanikio katika maisha yao.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, wazazi wengi wanakimbilia kuwapeleka watoto wao kufanyiwa vipimo hivyo katika jimbo la kaskazini la Shanxi. Taarifa hiyo imesema watoto wanaopelekwa kusomwa viganja ni kuanzia wenye umri wa miezi mitatu.
Kwa mujibu wa kampuni inayoendesha usomaji wa viganja iitwayo Shanxi Daomeng Communication, usomaji wa viganja unangamua ujanja na vipaji vya watoto.
Hata hivyo baadhi ya wataalam wametupilia mbali teknolojia hiyo ya kusoma viganja vya mikono. "Teknolojia hii inabakia kuwa bila ushahidi" Xinhua imemkariri mtaalam mmoja.
Utabiri na ubashiri, ikiwa ni pamoja na kusoma viganja vya mikono ya watu una mizizi ya muda mrefu katika utamaduni wa Uchina, ingawa viongozi wa nchi hiyo wamekuwa wakiwakata wananchi kutofuatilia na hata kutoa adhabu kali kwa watu wanaofanya shughuli hizo.
Watu wengi, ikiwa ni pamoja na maafisa wa serikali hutafuta ushauri wa wataalam wa kusoma nyota, umeripoti mtandao wa cnews.com.

ATAKA LIKIZO JELA

Beach
Angependa kwenda mahala kama hapa kupumzika
Mwanamama mmoja mwenye umri wa miaka thelathini na moja anayetumikia adhabu ya maisha jela nchini Sweden, amedai apewe likizo kutokana na kazi anayofanya gerezani humo.
Mtandao wa UPI.com umesema mwanamama huyo Natalia Pshenkina alifungwa kwa kukutwa na hatia ya kumuua rafiki wake wa kiume mwaka 2005.
Natalia alipatiwa kazi katika gereza la Ystad mwaka 2010 na anaamini anahitaji kupewa likizo yenye malipo, kwa mujibu wa sheria za kazi za Sweden, limeripoti gazeti la The Local.
Bi Natalia alimuandikia kansela wa sheria wa Sweden akiwasilisha malalamiko yake, inagwa alijibiwa kuwa hakuna likizo kwa wafungwa. Msemaji wa magereza wa Sweden, Anders Annerfalk amesema wafungwa wanaofanya kazi ndani ya magereza hawalindwi na sheria zinazowalinda wafanyakazi wengine.
"Kwa maana hiyo hakuna likizo" amesema.

WAFUNGWA WASHONA MIDOMO

Midomo
Wajishona midomo
Zaidi ya wafungwa elfu moja nchini Kyrgistan wameshona midomo yao, kupinga hali mbaya za magereza.
Hata hivyo mamlaka za huko zinasema magenge ya uhalifu ndio yanachochea hali hiyo ili waweze kutoroka gerezani.
Kyrgistan ni nchi iliyokuwa chini ya utawala wa kisovieti, na ina wananchi milioni tano, na wafungwa elfu saba na mia sita. Kwa miaka mingi kumekuwa na matendo yanayofanywa na wafungwa, lakini hili la Jumamosi iliyopita lilizidi kiwango.
Kwanza wafungwa wengi walifanya mgomo wa siku kumi wa kula. Lakini hatua ya kuishona midomo yao imekuwa ya kipekee kiasi cha kutikisa maafisa wa magereza.
Mwandishi mmoja wa habari wa AP alishuhudia baadhi ya wafungwa wakiwa wamejishona midomo huku wakiwa wamebakiza tundu dogo tu la kupitishia maji. Wafungwa hao wametumia nyuzi ngumu na hata waya kujishona.
Na kwa taarifa yako......
Bara pekee duniani lisilo na nyoka ni Antarctica

Milipuko yarindima Nigeria

 6 Februari, 2012 - Saa 22:53 GMT
Nigeria
Kumekuwa na mfululizo wa mashambulio nchini Nigeria
Kituo cha polisi kimeshambuliwa na mlipuko na kusakamwa na watu wenye bunduki katika mji wa kaskazini wa Kano na kujeruhi afisa mmoja wa polisi.
Upande wa mashariki, katika muda huohuo, watu walioshuhudia wamesema wamesikia milipuko katika soko la mji wa Maiduguri.
Hisia za nani aliyeandaa mashambulio haya zitaelekea kwa kundi wa wanamgambo la Boko Haram.
Boko Haram imeanzisha uasi katika eneo hilo katika jitihada za kuin'goa serikali ya nchi na kuanzisha taifa la Kiislam.
Kano ilishuhudia mfululizo wa mashambulizi mwezi uliopita yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 185.
Shambulio katika kituo cha polisi limetokea katika wilaya ya Sharada iliyopo Kano jioni ya saa kumi na mbili saa za huko.
Watu wenye silaha wakiwa na mabomu pia walikivamia kituo hicho kutoka pande mbalimbali, kwa mujibu wa msemaji wa polisi Magaji Musa Maji'a, akizungumza na shirika la habari la Reuters.
"Polisi mmoja alipigwa risasi mguuni na anapatiwa matibabu hospitalini," alisema.
Mkazi mmoja aitwaye Bala Salisu aliliambia shirika la habari la AFP kuwa alikuwa ndio kwanza ameingia nyumbani kwake kutekeleza amri ya kutotembea usiku aliposikia mlipuko mkubwa.
"Muda mfupi baadaye milio ya risasi ilisikika. Jinsi nilivyosikia ilikuwa kama wanajibizana kwa risasi," alisema.
Mwandishi wa habari wa Reuters katika eneo hilo amesema mlipuko ulikuwa na nguvu kiasi cha kutikisa madirisha, na kufuatiwa na mapambano ya risasi yaliyodumu kwa zaidi ya saa moja.
Magaji Musa Maji'a amesema maafisa wa polisi hatimaye walidhibiti hali ya kituo hicho.
Wakati huohuo katika mji wa Maiduguri - ambao ndio ngome ya Boko Haram - mfululizo wa milipuko imesikika katika eneo la sokoni na moshi mweusi ulionekana ukitanda katika eneo hilo.

WAGENI 43 KIZIMBANI MISRI!!!


NGO
Wafanyakazi wa kigeni Misri kufikishwa mahakamani

Baraza la kijeshi linalotawala Misri limetuhumu makundi ya kigeni kwa kusaidia kifedha maandamano ya mitaani dhidi ya utawala.
Baraza hilo lilivamia ofisi kadhaa za mashirika yasiyo ya kiserikali na kuwanyima ruhusa ya kusafiri wafanyakazi kadhaa wa kigeni kuondoka nchini humo.
Marekani imeonya kuwa itapitia upya misaada ya Marekani kwa Misri, ikiwa nchi hiyo haitaheshimu haki za mashirika yasiyo ya kiserikali.

Ufafanuzi

Msemaji wa serikali ya Marekani Victoria Nudland amesema Marekani "imepatwa na wasiwasi sana na taarifa hizo" na ilikuwa ikitafuta "ufafanuzi" kutoka kwa serikali ya Misri.
Kundi la wanaharakati wa haki za binaadam la Human Rights Watch limetoa wito kwa Misri kufuta mashtaka dhidi ya wafanyakazi hao wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
"Msaada kutoka nje ndio tegemeo lao. Serikali ya kijesi ya Misri sasa inatumia mbinu zilizotumika na Zimbabwe na Ethiopia kunyamazisha sauti huru," limesema kundi hilo.
Tangazo hilo limekuja katika siku ya nne ya ghasia mitaani nchini Misri huku kukiwa na hasira ya jinsi mamlaka zilivyoshindwa kukabiliana na matukio kwenye viwanja vya mpira wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 74.
Majeshi ya usalama yalirusha mabomu ya kutoa machozi kwa maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe huku wakielekea katika jengo la wizara ya mambo ya ndani mjini Cairo.
Wamarekani 19 ni miongoni mwa wanaoshtakiwa.

Fedha

Wanatuhumiwa kwa "kuunda matawi ya mashirika ya kimataifa nchini Misri bila ya leseni kutoka serikalini" na pia kwa "kupokea fedha kutoka nchi za nje kinyume cha sheria," limeripoti shirika la habari la AFP.
Mtoto wa waziri wa usafiri wa Marekani Ray LaHood anaaminiwa ni miongini mwa wanaokabiliwa na mashtaka hayo ya uhalifu.
Sam LaHood anaongoza ofisi ya shirika la IRI iliyopo Misri na ni miongoni mwa wafanyakazi kadhaa wa kigeni kunyimwa ruhusa ya kuondoka Misri, wiki moja iliyopita.
IRI na NDI, mashirika yanayohusishwa na vyama vya kisiasa vya Republican na Democrat vya Marekani, ni miongoni mwa mashirika 17 yanayopokea fedha kutoka nje na ambayo ofisi zao zilivamiwa na waendesha mashtaka mwezi Disemba.

Sunday, 5 February 2012

1ST ANNIVERSARY IN REMEMBRANCE OF, AIDA


We all miss you, Aida...R.I.P


Pongezi kwa wana Family...mambo yote yameenda sawa.




Huyo alie simama Steve mume wa malehemu mpendwa Aida. akiwa katika picha ya pamoja na
wana Family.

Hao wadada wawili hapo kati ni wadogo zake malehemu dada Aida.


Walio simama ni mama Paul na Steve..kama kunamtu hapa Leicester hamjui huyu mama.
basi mimi naamini ametoka magomeni jana.



Mapozi time kama kawaida kwa madada zangu



Wakubwa zangu hao, big up


Tupo pamoja dada zangu..alipangalo mungu hakuna wa kulipangua.




Bro Moses


Wanaiwakilisha vyema Leicester..Leicester oyeee