PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Saturday, 31 December 2011

TANGAZO KWA WADAU WOTE!!!

Mabadiliko ya jina la...kwanza entertainment blog.
Kwa sasa inaitwa, Nduguzangu
Unachotakiwa wewe ni kuiandika
Kama inavyo onekana hapa, anza na N kubwa
yaani kama hivi      Nduguzangu wala usiache nafasi Zote andika kwa pamoja....samahani sana kwa usumbufu utakao jitokeza,


Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2012
All the best kwa wadau wote popote mlipo
Asanteni sana, wenu papaya

Tuesday, 27 December 2011

CHEMSHA BONGO YA MERRY XMAS KWA WADAU!!!


Kuna £50 ya ubwete atakae sema wapi hapa bila ya kukosea...kazi kwenu wadau


Haya tena watu wa Leicester changamkia vijisent hapa £20 tu maana wenye njaa tambeee..
angalizo kwa wadau ninapo sema wenye njaa haina maana njaa ya chakula au pesa
bali ni njaa ya kujua ni wapi hasa hili jengo lilipo.


Wadau hapa cha £10 maana wenye njaa watakua wa kumwaga.


Monday, 26 December 2011

KWANZA ENTER, INATOA SALAAM ZA MERRY XMAS KWA WADAU WOTE POPOTE MLIPO.

Wadau hii kwa wote, najua fika kabisa ya kwamba mwaka huu XMAS imekuja wakati mgumu sana tena sana huku tukishuhudia uchumi ukiyumba dunia nzima, 




                                        Mwandishi wa kujitegemea
                                        Wa Kwanza Entertainment
                                         Anaejiita,( Papaya au He Tembo)


Ameota ndoto siku tatu zilizo pita kwa hiyo ameona bora aiweke hapa ili wadau waipitie kisha waichambue,


KWENYE BARA LA AFRICA AMEOTA NINI?
Hii hapa ndoto yenyewe.....watu wote wa vijijini ukitoa viongozi Wao wamekutwa katika vituo vya usafiri tena asubuhi kabisa Walipo ulizwa na viongozi wao vipi jamani mbona leo hivi? Mnaenda wapi wote kwa pamoja wamesema wanaenda kumuona Raisi wao kwakua wamechoka kuongopewa na viongozi wao..wale Viongozi walibaki midomo wazi huku wakijiuliza hao viongozi Kina nani kama sio sisi. Kisha mwandishi kamka toka usingizini.


habari ndio hiyo wadau...XMAS NJEEEMA kwenu.by He Tembo.

Saturday, 17 December 2011

HUYU ANAITWA SANAA LATHAN,FUATILIA CINEMA ZAKE UMUONE

Mwanadada anaetesa kwenye anga za cinema kule kwa obama
Hollywood kama analia vile

WADAU WA CINEMA JE MNAMJUA?!!! WESLEY SNIPES


CHELSEA TAABANI, YATOKA 1-1 NA WIGANI

Daniel Sturridge
Sturridge msimu huu ameifungia Chelsea magoli 9
Jordi Gomez alisawazisha baada ya dakika 87 na kupunguza kasi ya Chelsea katika juhudi za kufikia kilele cha ligi kuu ya Premier, na kuiwezesha timu yake ya Wigan kupata pointi muhimu katika kujinusuru kusalia katika ligi kuu.
Katika kipindi cha kwanza, Wigan walihisi walistahili kupata nafasi ya kupiga mkwaju wa penalti, baada ya mpira kutoka kwa Victor Moses kuugusa mkono wa Branislav Ivanovic.
Chelsea waliimarisha mchezo wao, na katika kipindi cha pili, Daniel Sturridge alitia mpira wavuni baada ya kupigiwa mpira na Ashley Cole.
Lakini Wigan hawakuogopa jina kubwa la Chelsea, na kufuatia mpira kumponyoka kipa Petr Cech, Gomez alitumbukiza mpira wavuni, na mechi kumalizika kwa sare ya 1-1.
Katika viwanja vingine, mechi za awali, Blackburn walishindwa magoli 2-1 walipocheza na West Brom.
Everton ilitoka sare ya 1-1 ilipokutana na Norwich.
Fulham ilithibitisha ngome ya Bolton bado ni dhaifu kwa kuwafunga magoli 2-0 kwa kirahisi.
Stoke iliishinda Wolves 2-1.
Mechi moja tu ndio ilikosa mabao, wakati Newcastle ilipocheza na Swansea, na wote kuondoka uwanjani 0-0.
Katika mechi za Jumapili, QPR itacheza na Man Utd, Aston Villa dhidi ya Liverpool, Tottenham iko uwanjani kupambana na Sunderland, na katika mechi inayotazamiwa kusisimua sana, Man City ikiongoza ligi itaikaribisha Arsenal.
Mechi hiyo ya kukamilisha mechi za Jumapili itaanza saa moja na dakika kumi jioni, kwa saa za Afrika Mashariki.
Ungana na Charles Hilary na Peter Musembi, ambao watakutangazia moja kwa moja mechi hiyo katika matangazo ya BBC ya Ulimwengu wa Soka, kuanzia saa kumi na mbili na nusu jioni, saa za Afrika Mashariki.

Sunday, 4 December 2011