Wafungwa 1,000 watoroka gereza la Congo
Takriban wafungwa 1,000 wametoroka gerezani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha, maafisa wamesema.
Waziri wa habari Dkianga Kazadi alisema washambuliaji hao walitaka kumwachia huru kiongozi wa wapiganaji, katika jimbo la Katanga.
Utorokaji na uasi ni jambo la kawaida kutokea kwenye magereza ya Congo, wachambuzi wanasema, upande wa mashariki ukiwa haufuati sheria huku wapiganaji wa upinzani wakigombea utawala.
Takriban wafungwa 200 walitoroka kwenye gereza lililopo kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo mwaka jana.
Bw Kazadi alisema watu wenye silaha waliofunika sura zao waliingia kwenye gereza la mjini Lubumbashi bila mtu kuwatambua.
Kulingana na shirika la habari la AFP, alisema "Waliwafyatulia risasi polisi na walinzi, na kuua wawili."
Msemaji wa umoja wa mataifa Congo, Madnodje Mounoubai, aliiambia BBC aliyekuwa kamanda wa wapiganaji wa Mai Mai, Gedeon Kyungu Mutanga, alitoroka.
Mutanga alihukumiwa kifo mwaka 2009 kwa kujihusisha na ghasia zilizochukua muda mrefu mashariki mwa Congo.
Bw Kazadi alisema polisi wamewakamata upya wafungwa 152 kati ya 967 waliotoroka
No comments:
Post a Comment