Feri yazama Zanzibar, 'mamia' wafariki
Mamia ya watu wanahofiwa kufariki dunia baada ya feri kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania ikiwa imewabeba zaidi ya watu mia tano.
Zaidi ya watu arobaini na tatu wameaga dunia katika mkasa huo , mmoja wa mawaziri katika kisiwa hicho kinachojitawala amesema.
Takriban watu 260 wameripotiwa kuokolewa
Feri hiyo MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya kisiwa kikubwa zaidi cha Unguja ikielekea Pemba ambacho pia ni kisiwa cha Zanzibar.
Hadi kufikia sasa tumeopoa miili 43, lakini tumewaokoa manusura 259
Mohammed Aboud, waziri anayehusika na maswala ya dharura Zanzibar.
" ," amesema Mohammed Aboud, waziri wa Zanzibar anayehusika na mikasa. Ameongeza kuwa 40 kati ya wale waliookolewa walikuwa na mejeraha mabaya.
Likizo ya Ramadhan
Feri hiyo iliondoka Unguja saa nne usiku na inasemekana kuzama majira ya saa saba usiku.
Shirika la habari la AP limeripoti kwamba feri hiyo ilikuwa imebeba abiria kupita kiasi.
Ilikuwa ikiwarejesha watu waliokuwa likizo ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na watoto wengi walikuwa miongoni mwa abiria hao.
Mwandishi wa BBC aliyepo Zanzibar amesema miili mingi imeanza kuelea na kusukumwa ufuoni na maafisa wanakabiliwa na kibarua kigumu kuushughulikia mkasa huo.
Maafisa wametenga eneo maalum la uokoaji na kutoa wito kw amataifa mengine ya Afrika kutoa msaada wa vifaa maalum vya uokoaji.
No comments:
Post a Comment