PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Thursday, 25 August 2011

TANZANIA YAPIGA STEP

RAIS Jakaya Kikwete amezindua nembo yenye kuhamasisha matumizi ya mabadiliko ya analojia kwenda digitali kwa lengo la kuboresha matangazo kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano nchini.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Shirika la Mawasiliano la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CTO) kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 250, umeandaliwa na shirika hilo kwa pamoja na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ukiwa na maudhui ya kuboresha maisha ya wananchi wa vijijini kwa kuwaunganisha na teknolojia ya mawasiliano.

Awali, akizungumza kuhusu mkutano huo, Rais Kikwete alisema matumizi ya Teknolojia ya Habari (ICT) yanahusisha dunia katika kuleta maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kuhamasisha kukua kwa uchumi na kuimarisha ubunifu katika vifaa mbalimbali.

Rais Kikwete alisema jamii ya Afrika inasubiria matumizi ya teknolojia hiyo pamoja na kuona matunda yake ambapo sera mbalimbali, taratibu na sheria kuhusu uwekezaji katika sekta hiyo zitawezesha kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Alisema maudhui ya mkutano huo yamekuja kwa wakati muafaka kwa jamii ya nchi za Afrika ambapo kuunganisha wananchi wa vijijini na teknolojia hiyo imebaki kuwa na changamoto.

Aidha, alisema hadi sasa tayari kilometa 7,000 zimeshatekelezwa katika Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa na kati ya kilometa 10,000 zilizopangwa kufikiwa kwa awamu ya kwanza na utakapokamilika utaunganisha mikoa na wilaya mbalimbali na kusaidia kufikia MDGs.

“Ipo haja ya kuhamasisha matumizi ya ICT kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2025. Sera ya Taifa ya ICT inalenga kuifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha teknolojia hiyo na kuwa suluhu ya maendeleo ya uchumi na kupunguza umasikini,” alisema Rais Kikwete.

Akifafanua kuhusu uzinduzi wa nembo hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa alisema mkakati huo umeanza sasa hivi na kwamba inategemewa kufikiwa mwakani, Tanzania iwe imebadilika kabisa kwa matumizi hayo.

Alisema faida ya kutumia mfumo wa digitali ni pamoja na kuboresha matangazo mbalimbali
yatolewa nchini na kutoa fursa nzuri ya kutumia masafa marefu katika teknolojia ya mawasiliano.

No comments:

Post a Comment