PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Saturday, 20 August 2011


Kufutari

Waisilam wanaoishi katika jengo refu zaidi duniani, wanalazimika kusubiri muda zaidi kufutari kuliko waisilam wengine, kwa kuwa jua linachelewa kuzama huko walipo, kutokana na urefu wa jengo hilo.
Jengo hilo liitwalo Burj Khalifa liko Dubai.
Kiongozi wa juu wa kidini wa Dubai, Mohammed al-Qubaisi amesema wale wanaoishi zaidi ya ghorofa ya themanini, lazima wasubiri dakika mbili zaidi, baada ya muda kutimia mjini Dubai ili kupata futari yao.
Mwezi wa Ramadhani ulianza wiki moja iliyopita.
Gazeti la Mirror limesema shekhe huyo amesema wale wanaoishi katika ghorofa ya mia moja na hamsini na kuendelea, watalazimika kusubiri dakika tau zaidi ya wenzao.
Jengo hilo, Burj Khalifa, lina ghorofa mia moja na sitini. Waisilam huanza kula futari mara wanapoona jua limezama

No comments:

Post a Comment