PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Friday, 21 October 2011

SERIKALI YAWEKA UTARATIBU KUPOKEA, CHENJI YA RADA

Serikali kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID), inafanya utaratibu wa kupokea Paund milioni 29.50 (Sh. bilioni 75) zikiwa ni malipo ya fedha za tozo za rada.
Pia inafanya utaratibu wa kushughulikia akaunti itakayotumika kuhifadhi fedha hizo zitakapoingia nchini.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE.
Alisema utaratibu huo unafanyika baada ya Serikali ya Uingereza kuihakikishia Serikali ya Tanzania kwa maandishi kwamba, italipwa fedha hizo.
Mkulo alisema hayo alipotakiwa na NIPSHE kueleza kama Serikali ya Tanzania imekwisha kupokea fedha hizo au la.
“Tumeshapata barua kutoka Serikali ya Uingereza kwamba, serikali (ya Tanzania) italipwa Paund milioni 29.50,” alisema Waziri Mkulo.
Alisema utaratibu huo unafanywa kati ya serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Fedha na Uchumi, BoT na DFID.
Fedha hizo zinarejeshwa nchini baada ya Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza iliyouzia Tanzania rada hiyo kwa bei kubwa kuliko bei yake halisi, kuamriwa na mahakama nchini humo, kulipa faini hiyo.
Amri hiyo ilitolewa na mahakama, baada ya kampuni hiyo kugundulika kwamba, ilikwenda kinyume katika kuiuzia Tanzania rada hiyo mwishoni mwa miaka ya 1990.
BAE iliiuzia Tanzania rada hiyo kwa dola za Marekani milioni 40 (Sh. bilioni 54), hatua iliyopingwa na wengi, akiwamo aliyekuwa Waziri wa Uingereza wa Masuala ya Afrika, Clear Shot, aliyejiuzulu, pamoja na taasisi mbalimbali, ikiwamo Benki ya Dunia (WB).Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

No comments:

Post a Comment