NILIPOACHISHWA kazi nilichanganyikiwa na kudhani ndio mwisho wa maisha…lakini tatizo
la ukosefu wa ajira kwa vijana ulinipa msukumo wa kuanzisha chuo cha ufundi stadi na kutumia elimu na ujuzi wangu kuendelea kulitumikia taifa kupitia sekta binafsi,” anasema Karoli Stephen.
Stephen ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa chuo cha ufundi stadi kinachojulikana kama Metro Institute of Technology kilichopo Tanga, alianzisha chuo hicho baada ya kupoteza ajira yake serikalini mwaka 1999.
Awali Stephen alikuwa Mkufunzi katika Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kituo cha Tanga na baada ya kuachishwa kazi, wanafunzi kutoka viwandani na vyuoni walikuwa wakimfuata na kumuomba awafundishe kwa kuwa hawakuwa na mwalimu.
“Nilipowaambia sina pa kufundishia waliamua kukodi darasa kisha kunisihi nikawafundishe kwa sharti la kuwatoza kiasi kidogo cha ada ili niweze kulipia pango na kujikimu,” anasema.
Baada ya kupata changamoto hiyo, mwaka 2000 alifanikiwa kupanga katika jengo la CCM lililopo eneo maarufu kwa jina la Kwa Kwaminchi na kuanzisha chuo alichokiita Amani Training Institute.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye alijikuta akilazimika kulihama eneo hilo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wanamimimika kupata elimu ya ufundi stadi. Mwaka 2001 alihamia majengo ya NMC Gofu kisha kuunganisha nguvu ya taasisi mbili yaani Amani Training Institute na Nyerere Youth Centre, muungano uliozaa chuo cha Metro Institute of technology.
Umati wa wanafunzi walioendelea kumiminika kwenye chuo chake ulimpa wakati mgumu, kiasi
cha kuanza mchakato wa kutafuta eneo kubwa zaidi. Akiwa katika mchakato huo, mwaka 2007 alilazimika kufunga chuo hicho kwa muda.
Alikifungua tena mwaka 2010 baada ya kupata eneo kubwa katika moja ya majengo ya Bandari ya Tanga ambako ameyaboresha baada ya kuingia nao mkataba wa muda mrefu.
Anakiri kwamba, kwa sasa ana eneo kubwa, hivyo kuwafanya wanafunzi kujifunza fani zaidi ya
kumi bila ya kulazimika kubanana.
“Tumefanikiwa kuongeza idadi ya fani hadi kufikia kumi ambazo ni ufundi magari, umeme wa magari, uungaji wa vyuma, useremala, uashi, umeme wa majumbani, udereva, kompyuta, ushonaji wa nguo na upambaji,” alisema na kuongeza kuwa, chuo kimejikita katika fani mbalimbali ili kuwapa vijana fursa ya kujiendeleza na kuweza kujiajiri baada ya kuhitimu.
Anasema: “Tatizo la ukosefu ajira kwa vijana limekuwa kubwa na ni bomu linaloweza kulipuka
wakati wowote hivyo chuo kimeamua kushirikiana na wadau wengine kupunguza tatizo hilo kwa kutoa elimu ya ufundi stadi na kuhimiza vijana wajiajiri.”
Ili kuondokana na kero inayowapata wahitimu wanaokosa ajira kwa kisingizio cha kukosa uzoefu, chuo hicho kimeweka mpango unaowawezesha wanafunzi kwenda maeneo mbalimbali kufanyakazi ili kuimarisha mafunzo kwa vitendo na kupata uzoefu katika fani ya umeme wa majumbani, kompyuta na mapambo.
“Dhamira ya chuo hiki ni kuhakikisha vijana wananufaika na elimu ya ufundi ili kuwa chachu ya maendeleo katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kwani bado tupo nyuma sana katika elimu ya ufundi” anasema,” Stephen ambaye chuo chake kinatoa mafunzo muda mfupi na muda mrefu.
Muda mrefu ni pamoja na ile ya mwaka mmoja inayojumuisha mafunzo ya udereva na ufundi ambazo humuwezesha mwanafunzi kufanya mitihani ya Trade Test na CBE inayotolewa na VETA.
Kozi ambazo zinachukua mwezi mmoja na nusu na zile za wiki mbili ni pamoja na udereva wa awali na mafunzo ya kompyuta kwa wale wanaojiendeleza bila kufanya mitihani ya VETA.
Chuo hicho kimefanikiwa kuongeza kiwango cha ufaulu katika programu za mitihani ya Trade
Test inayotolewa na VETA, ambapo ufaulu huo umeongezeka hadi kufikia asilimia 82.3 ya wanafunzi wote walioandikishwa.
Ufanisi huo unatokana na mkakati wa chuo wa kukuza kiwango cha ufaulu kwa kuajiri walimu
wenye elimu na uzoefu wa kutosha katika nyanja mbalimbali, miundombinu mizuri, na vitendea kazi vya kutosha ikiwa ni pamoja na magari ya mafunzo ya udereva na zana za ufundi.
Pia chuo hicho kinatumia kaulimbiu inayosema “Umahiri unaouzika” ikiwa na maana ya
kuongeza elimu na maarifa ili kuibua vipaji na mambo halisi ambayo hayafahamiki katika ufundi stadi.
Anasema ufaulu wa mitihani kwa wanafunzi wa chuo hicho unatokana na ushindani wa kuonesha kwa vitendo uwezo na umahiri wa kila mwanafunzi kudhihirisha kama alielewa ipasavyo mafunzo ya nadharia na kutumia elimu yake kutatua matatizo kwa kutumia fani au
ufundi stadi.
“Hatutaki mwanafunzi ahitimu katika chuo chetu akiwa na chochote alichojifunza, bali atoke akiwa ameiva na kumudu ushindani wa soko la ajira kwa kufanyakazi kwa umahiri wa kiwango cha juu,” anasema Stephen.
Mkurugenzi huyo aliyeonesha mfano wa kutokata tamaa baada ya kupata matatizo, ikiwa pamoja na kufukuzwa kazi, anasema chuo chake kwa sasa kinakabiliwa na changamoto ya kukamilisha azma ya kutekeleza kauli mbiu ya ujuzi unaouzika kwa kuwa maendeleo ya
sayansi na teknolojia yanakwenda kwa kasi ikilinganishwa na mabadiliko ya mitaala ya mafunzo ya ufundi pamoja na masharti ya kisheria ambayo yanalazimisha kufuata mitaala
inayotolewa na mamlaka ya elimu ya ufundi stadi.
Ameitaja changamoto nyingine kuwa ni gharama kubwa ya mafunzo ya ufundi stadi akisema elimu ya vitendo inahitaji vifaa vya kisasa ambavyo wanafunzi wa familia ya kipato cha chini haiwezi kumudu kuvinunua.
Kutokana na hali hiyo, anasema hali hiyo inachangia kukwamisha jitihada za chuo hicho kufikia malengo waliyonayo hivyo wanaiomba Serikali, wafadhili na wadau na katika maendeleo ya ufundi wajitokeze ili kukisaidia chuo hicho kiweze kuondokana na changamoto
hizo.
Stephen anasema pamoja na changamoto mbalimbali, chuo chake kinaweka mikakati ya kupanua huduma na katika miaka mitano ijayo kitakuwa na uwezo wa kusajili wanafunzi 600 kwa mwaka badala ya wanafunzi 100 wa sasa.
Pia chuo hicho kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kina mkakati wa kutoa mafunzo ya elimu ya sekondari hususani kwa watu wazima wanaotaka kufanya mitihani ya kidato cha nne na sita.
Anasema chuo chake kimefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa kuna watu wengi wanaotaka kufanya mitihani ya sekondari ili kuboresha viwango vyao vya elimu. Anawahimiza watu wenye elimu na uwezo wa kuchangia taifa wasisubiri kuajiriwa serikalini badala yake wajiunge na sekta binafsi kwa kujiajiri wenyewe na kuajiri watu wengine kwa kuwa jambo hilo linawezekana.
Stephen amepata elimu ya awali katika shule ya msingi katika Shule ya Msingi Ndekeli mwaka
1979 na kujiunga Shule ya Ufundi Ifunda, mkoani Iringa ambako alihitimu mwaka 1983 na baadaye alisoma Chuo cha Ufundi Arusha alikohitimu mwaka 1986.
Miaka minne baadaye aliajiriwa na Ofisi ya Rais, Idara Kuu ya Utumishi na kupangiwa kufanya kazi Wizara ya Kazi hadi mwaka 1993 alipopata fursa ya kujiunga na Chuo cha Chang’ombe, Idara ya Taifa ya Mafunzo ya Ufundi Chang’ombe (NVTD) kuchukua mafunzo ya ualimu.
Ingawa Stephen amejikita katika ufundi anapenda kujishughulisha na kilimo,kusoma, kujifunza
maandiko matakatifu katika biblia na kufanya mazoezi.

No comments:
Post a Comment