MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama ameanza kupewa orodha ya watumishi
wanaokula rushwa na mgawo wa rushwa kulingana na nafasi zao katika utumishi wa umma mkoani humo.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Gama alisema baada ya kutoa namba ya simu yake ya mkononi kwa wananchi wa wilaya za Rombo na Same, amepata taarifa zilizomsaidia kufahamu utendaji wa viongozi hao na udhaifu wao.
“Tangu nimetoa namba za simu nimepokea tuhuma nzito za viongozi wa wilaya, hususani ya Rombo… nimepewa orodha ya wala rushwa na wamegawanywa kwa makundi na nafasi zao kuna wa Sh 50,000, 100,000 na 500,000 sasa mwisho wao umefika,” alisema.
Alisema kitendo cha wananchi na wafanyabiashara wasio waaminifu kununua vyombo vya
dola ni udhalilishwaji kwa Serikali na sasa mwisho wake umefika kwa kuwa amekusudia kuusafisha mkoa huo.
“Niliyoelezwa kuhusu wilaya ya Rombo yanatisha, sasa sitavumilia kama kuna watumishi wanadhani hawawezi kazi waache…hii nchi ina wasomi wengi sana, tukikuondoa wewe, nafasi yako itagombewa na watu siyo chini ya 200,” alisema.
Alisema amekwenda katika mkoa huo kuhakikisha maagizo na maelekezo ya Serikali
yanatekelezwa, hivyo mtumishi yeyote ambaye hawezi kusaidia shughuli za maendeleo kulingana na maadili ya utumishi, atafukuzwa kazi.
“Nikishatembelea wilaya zote, nitawaita watumishi katika idara zote ikiwemo Polisi, Mamlaka ya Mapato (TRA), watumishi wa afya, elimu, barabara na wengineo, ninataka kuwaeleza kuwa mwenye kutaka kazi afuate maadili, vinginevyo aziache ofisi za umma wazi,” alisema.
Awali Meneja wa Skimu ya Umwagiliaji wa Mpunga ya Ndungu, Beda Mtungi alisema mwaka
huu Shirika la Chakula Duniani (FAO) limeipatia kijiji cha Ndungu mbegu bora za mpunga aina ya TXD-306 tani 11.8.
Pamoja na shirika hilo lakini pia Serikali kwa mwaka 2010/2011 imesambaza vocha zipatazo 900 za mbegu bora ya mpunga aina ya Saro 5, mbolea ya kupandia na mbolea ya kukuzia
No comments:
Post a Comment