PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Thursday, 20 October 2011

NAPE, CCM SI KICHAKA CHA MAFISADI

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema chama hicho si kichaka cha kujifichia mafisadi na viongozi wabovu na wabadhirifu na kwamba wanaodhani watafanikiwa kukigeuza chama hicho kichaka wanajidanganya.

Nape aliyasema hayo jijini Mwanza jana wakati akihutubia mkutano kwenye Viwanja vya Igoma Sokoni ulioandaliwa na chama hicho katika mwendelezo wa ziara ya baadhi ya viongozi wa kitaifa wa CCM Kanda ya Ziwa iliyoanza tangu juzi.

Akitumia mifano kadhaa ya Biblia na Korani, Nape alisema hata Bwana Yesu alipokuta wafanyabiashara wanageuza nyumba ya Baba yake pango la walanguzi, aliwakemea na kuwafukuza, hivyo naye anachofanya ni kusafisha chama ili kisigeuzwe kichaka cha kujifichia waovu.

“Yesu alikwenda hekaluni na kuwaambia wafanyabiashara nyumba ya Baba yangu itakuwa nyumba ya sala na si pango la wanyang'anyi, akapindua meza zao na kuwafukuza kwa ukali, leo Nape akikemea maovu ndani ya chama mnataka kumtoa roho? Sitishiki Mungu yuko upande wangu na ndio maamuzi ya chama changu, nami nayaamini,” alisisitiza Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi.

Aliwashangaa baadhi ya viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya kujilimbikizia mali wakiwajibika serikalini wanaenda kujificha kwenye chama, akihoji kuwa tabia hiyo ni kukigeuza chama kuwa kichaka cha waovu na hivyo kukifanya chama kupoteza imani yake kwa wananchi.

“Kama wanaoonekana serikalini hawafai, au kwenye mashirika ya umma wameshiriki kuyaua, hapa Mwanza mfano mzuri ni waliokifikisha Chama cha Ushirika Nyanza kilipo leo, halafu hao ndio tunawakumbatia na kuwapa nafasi kwenye chama nani atatuamini?”

Alihoji Nape. Alisema alishawahi kutangaza huko nyuma, hivyo anarudia Mwanza kuwa wale walioshiriki kwa namna moja ama nyingine na hujuma kwa Chama cha Ushirika Nyanza, uchaguzi wa mwakani wa CCM wasichukue fomu za kugombea nafasi yoyote kwani matendo hayo yanatosha kuwapotezea sifa ya kuwa viongozi wa chama.

Aidha, Nape amesema ipo haja sasa kujadili kwa kina namna ya kupunguza tofauti kubwa ya kipato iliyopo kati ya masikini na matajiri kwani ni hatari kwa amani ya nchi

No comments:

Post a Comment