MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi ametoa mwito kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini kuchukia rushwa kama njia ya kupunguza tatizo hilo nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wazo Hill, Mengi alisema wanafunzi wanatakiwa kufahamu kuwa aliyetoa na kupokea rushwa wote wana hatia na wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema wanafunzi hao wakichukia rushwa, wawaambie wazazi wao pia kuwa inatosha kuwa na Taifa ambalo baadhi ya watu ndio wanafaidi raslimali za umma na kuwaacha wengine wakiwa masikini.
“Waambieni wazazi wenu kuwa imetosha, lakini cha muhimu kwanza wewe mwenyewe chukia rushwa.
“Kuna Watanzania wengi tu ambao wanafungwa kwa kuiba kuku, ila wanaoiba mamilioni ya fedha hawafungwi,” alisema Mengi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule hiyo, Valence Misaki alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa maabara.
Lakini alimshukuru Mengi ambaye aliahidi kuisaidia shule hiyo kiasi cha Sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo.
No comments:
Post a Comment