Sunday, 2 October 2011


Waandamanaji wazinga Wall Street

Polisi mjini New York wamewakamata watu zaidi ya 700 ambao walizinga daraja moja ya mji huo iitwayo Brooklyn Bridge, walipoandamana kupinga kile wanachokiona kama uroho wa wafanya biashara ya fedha.
Waandamanaji wa New York
Afisa wa serikali alisema walikamatwa kwa sababu walizinga magari kupita.
Waandanamanaji hao, kwa majuma mawili, walikuwa karibu na barabara ya masoko ya fedha, Wall Street.
Wanaharakati hao wanaojiita "Anti-Wall street", yaani "wapinzani wa Wall Sreet", kwanza walikuwa kwenye bustani ndogo mjini humo kwa wiki mbili, kupinga fedha zilizotumika kusaidia mabenki mwaka 2008, na ushawishi mkubwa wa makampuni kwenye siasa za nchi.
Kikundi cha internet, kiitwacho Adbusters, ndicho kilichopanga mkusanyiko huo.
Kikundi kiitwacho "Occupy Wall Street" kina wafuasi tofauti, wanasema wamevutiwa na harakati za jamii za Uspania na vuguvugu la nchi za Kiarabu.
Wana biramu zinazoonesha malengo yao - kama kuwalenga wanaopendelewa na mfumo wa kodi, uroho wa makampuni na wanataka amani.
Piya wanapinga utumizi wa nguvu na kile wanachoona kuwa ukosefu wa haki kwa wachache, wakiwemo Waislamu.
Wanaharakati hao piya wanapinga watu kunyang'anywa nyumba zao, kwa sababu wameshindwa kulipa deni la nyumba, ukosefu wa kazi, na serikali kuyasaidia mabenki mwaka wa 2008.
Watu wa filamu, kama Michael Moore na mchezaji sinema, Susan Sarandon, walipita kuwaunga mkono waandamanaji.
Kikundi hicho sasa kimeanza kupata wafuasi katika miji mengine mikubwa ya Marekani.

No comments:

Post a Comment