Monday, 3 October 2011


ICC yataka uchunguzi Ivory Coast

Moreno Ocampo
Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imempa idhini mkuu wake wa mashtaka kuanza uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa Ivory Coast.
Watu wapatao 3,000 waliuawa na wengine 500,000 kuachwa bila makao katika ghasia hizo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Alassane Ouattara alichukuwa hatamu za uwongozi mwezi Aprili baada ya miezi minne ya mvutano na mwenzake Laurent Gbagbo aliyekataa kukubali ushindi wa Ouattara.
Vikosi tiifu kwa mabwana hawa wawili vyote vimeshutumiwa kwa uhalifu na ukiukaji haki za binadamu.
Majaji wa ICC pia walimtaka mkuu huyo wa mashtaka Luis Moreno-Ocampo, atoe majibu ya uchunguzi wake katika kipindi cha mwezi mmoja kuhusu taarifa zaidi za uhalifu zilizotekelezwa kati ya mwaka 2002 na 2010.
Uchaguzi wa mwezi November ulinuiwa kuwaleta pamoja wananchi na kuiunganisha nchi hiyo iliyogawanywa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002.
Ivory Coast - mzalishaji mkubwa wa zao la Kakao duniani- ilionekana wakati mmoja kuwa eneo la amani na ufanisi la Afrika Magharibi .
Nchi hiyo wakati huu inaonekana kukabiliana na mgawanyiko na pasuko unaozingatia ukabila, dini na uchumi.
Bw Gbagbo wakati huu anahudumia kifungo cha nyumbani na ameshtakiwa na uporaji maji , wizi wa kutumia nguvu na ufujaji mali.
Alikataa kata kata kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Rais, licha ya Umoja wa Mataifa kumtangaza Bw Ouattara adui wake wa jadi kuwa mshindi.

No comments:

Post a Comment