PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Wednesday, 5 October 2011

Image
USALAMA na amani ni vitu muhimu katika maisha ya binadamu yeyote na taifa kwa ujumla.

Kuwepo kwa vitu hivyo huwafanya wananchi kuendesha maisha yao ya kila siku na kuzalisha mali ili kujiongezea kipato. Moja ya mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya wananchi ni vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani, ambavyo husababisha uharibifu na upotevu wa mali kwa raia.

Kila mmoja wetu anatambua kuwa Jeshi la Polisi ndilo lenye jukumu kubwa la kulinda raia na mali zake, lakini kila raia ana wajibu wa kumlinda mwenzake kwa kushirikiana na polisi.
Wananchi watatoa ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi, wanaweza kutokomeza vitendo vya uhalifu, uvunjifu wa amani na mauaji, kutokana na jamii kuwatambua wahalifu.

Ili kufanikisha azma ya wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kuwa na imani na chombo hicho, Chuo cha Taaluma ya Polisi cha Mjini Moshi, ambacho huku nyuma kilitambulika kama CCP, kimeanza kutoa mafuzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaozalishwa chuoni hapo.

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi, Matanga Mbushi, anasema ili
kuhakikisha Jeshi la Polisi na wananchi wanashirikiana, chuo hicho kimebadilisha mfumo wa mafunzo kutoka ule wa nadharia (KBET) kwenda kwenye mfumo wa vitendo (CBET), kwa kuwapeleka askari Polisi kwa wananchi, lengo likiwa ni kujifunza jinsi ya kushirikiana nao katika usalama.

Mbushi anasema kutokana na mabadiliko hayo, inabidi kuwapeleka wanafunzi katika kufanya yale waliyoyasoma kwa nadharia kwenda kufanya kwa vitendo kwa kushirikiana na wananchi, ambapo itakuwa moja ya sehemu ya mitihani yao, lengo likiwa ni kutambua jinsi ya kushirikiana na raia ili wawe na imani na Jeshi la Polisi.

Anasema lengo la kubadilisha mfumo wa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea uaskari chuoni hapo, ni kukidhi mahitaji ya Jeshi la Polisi ambayo yanalenga kutoa askari wemye weledi, usasa na wenye uwezo wa kutekeleza falsafa ya Polisi Jamii kwa vitendo.

“Huu ni mkakati maalumu uliopangwa kama sehemu ya utekelezaji wa kazi kwa maboresho
ya Jeshi la Polisi, ambapo itasaidia Polisi kutambua matatizo na kero za wananchi zinazowakabili katika uhalifu na kuhakikisha jamii inashirikiana na kuwa na imani na Jeshi la Polisi”, anasema Mbushi.

Mbushi anasema ulinzi ngazi ya Kata, kwa sasa ndo mpango mkakati wa ulinzi shirikishi na Polisi Jamii.

Lengo lake ni kuongeza ufanisi na tija kwa Jeshi la Polisi katika kutoa huduma bora kwa wananchi, kwa kuzuia na kupambana na uhalifu Mkuu huyo wa Chuo anasema kuwa katika awamu hii ya kwanza, kuna wanafunzi 632 ambapo 94 ni wanawake na wanaume 538, wanaosomea mafunzo kwa mfumo wa vitendo katika wilaya za Hai na Siha mkoani Kilimanjaro na Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Anasema kuwa wanafunzi hao wanapopelekwa uraiani ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo kabla ya kuhitimu, watakuwa wakitoa elimu kwa wananchi, juu ya umuhimu wa kuwa na Polisi Jamii, na ushirikiano kati ya polisi na raia ili kutokomeza vitendo vya uhalifu.

Anasema m a f u n z o hayo, yamea n d a l i w a kwa madhumuni ya k u w a j e n g e a uwezo wa kiutendaji Jeshi la Polisi, juu ya kubaini na kuzuia uhalifu kwa kushirikiana na jamii. Mbushi anasema jamii inapokuwa karibu na Jeshi la Polisi, ina k u w a rahisi zaidi kutoa ushirikiano wa haraka katika kukabiliana na kuzuia uhalifu, kwani wahalifu wapo miongoni mwa hiyo jamii.

Mbushi anasema kuwa kila mwanafunzi chuoni hapo, atapata mafunzo ya vitendo kwa kupangiwa vituo mbalimbali ili kutoa elimu juu ya ulinzi shirikishi na Polisi Jamii na kutambua matatizo yanayowakabili wananchi.

Anasema mafunzo yatakayokuwa yakitolewa kwa wananchi ni pamoja na kutoa elimu ya muundo wa kamati za ulinzi na usalama wa kata, sheria za mamlaka za Serikali za Mitaa na utendaji kazi wa askari Polisi wasaidizi katika kusimamia ulinzi na usalama.

Mbushi anasema kuwa mafunzo mengine wanayoyapata wananchi kutoka kwa wanafunzi wa uaskari chuoni hapo ni matumizi ya taarifa za kiintelijensia katika utendaji kazi wa polisi ili kubaini na kuzuia uhalifu kwa ushirikiano wa jamii katika himaya.

Mafunzo mengine ni jinsi ya kuhamasisha wadau wengine kuwa wabia katika ulinzi na
usalama kwenye himaya ili kupata rasilimali katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu na mazingira ya ukamataji salama ili kuzuia madhara katika tukio.

Pia, Mbushi anasema wananchi wanapatiwa elimu ya utekelezaji wa huduma bora kwa mteja na mawasiliano ndani ya Jeshi la Polisi kulingana na miongozo, taratibu, kanuni na nyaraka
m b a l i m - b a l i , na utii wa sheria.

“Mpango mkakati huo utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, hivyo kuondoa dhana potofu za hapo awali, ambapo raia walikuwa wakiwaogopa askari bila hata ya kufanya kosa, hali iliyokuwa ikisababisha polisi kutokuwa na ushirikiano na raia “ anasema.

Anasema kuwa kitendo cha askari kuwa karibu na wananchi, kitawajengea uwezo wa kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu, kwa kushirikiana na jamii husika ambayo huwa karibu na watu wanaofanya matukio hayo.

Mbushi anasema kuwa Chuo hicho kitahakikisha kinazalisha askari wenye weledi na waliobobea kutokana na mafunzo ya vitendo, hivyo itakuwa rahisi kwenda kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi, kutokana na mafunzo wanayoyapata.

Katika kuhakikisha askari hao wanaiva vizuri kwa lengo la kutatua matatizo ya wananchi na kumaliza uhalifu, uvunjifu wa amani na mauaji, Kamishna wa Polisi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi, Nasser Mwakamboja, anasema mafunzo wanayoyapata wanafunzi chuoni hapo, yatasaidia wananchi kuwa na imani na jeshi hilo.

Mwakamboja anasema kuwa wanafunzi wanaomaliza chuoni hapo baada ya kupata mafunzo ya vitendo, watapangiwa kwenye vituo na watafanya kazi na wananchi, kama wakuu wa vituo wasaidizi katika tarafa, ambapo Mwenyekiti wa Kamati atakuwa Ofisa Mtendaji wa Kata, na Katibu wake Mkuu wa Kituo cha Polisi wa eneo husika (OCD).

Anasema kuwa wanapeleka wanafunzi wa uaskari kujifunza mbinu za kuwa karibu na kupata ushirikiano kwa wananchi, kwa lengo la kujenga motisha na ari ya wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutatua matatizo ya jamii hususani ya ulinzi na usalama.

“Tunatarajia kuwa mafunzo haya, yatasaidia kutambua mchango wa wadau mamlaka na majukumu ya viongozi waliopo katika jamii. Kushirikiana nao ipasavyo kutasaidia kubaini kuzuia na kukabiliana na uhalifu unaofanywa na wahalifu, ambao hutambuliwa na jamii lakini hushindwa kubainika, kutokana na kutokuwepo kwa ushirikiano”alisema Kamishna Mwakamboja.

Mwakamboja anasema kuwa mafunzo hayo pia yanazingatia utawala bora katika himaya na kutafuta misingi ya sheria, pamoja na kujikita zaidi kwenye upolisi wa kubaini na kuzuia uhalifu kwa kushirikiana na jamii na kuondokana na upolisi wa kupambana na matukio baada ya kutendeka.

Kwa upande wao askari Polisi wanafunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi, Edward
Mwalimu na Arulike Leonard, wanasema ili kufanikisha mpango huo, viongozi wa dini wanatakiwa kutoa mchango wao katika kuwajenga waumini wa dini zao kiimani zaidi ili waogope kufanya uhalifu.

Mwalimu na Leonard wanataja baadhi ya vyombo ambavyo vikitumika vizuri, vitapunguza uvunjifu wa amani na kila mmoja kuwa na uelewa juu ya kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Vyombo hivyo ni vyama vya siasa, vyombo vya habari na Mahakama. Vyama vya siasa vitaweza kuwalea wanachama katika mazingira ya amani na Mahakama zitaweza kutoa haki
mtu anapokutwa ana makosa

No comments:

Post a Comment