Umoja wa Mataifa unasema inatafuta kurejesha mali yenye thamani zaidi ya dola milioni sabini kutoka kwa mtoto wa Rais wa Equatorial Guinea.
Teodoro Obiang NguemaKitengo cha haki nchini Marekani kinamshutumu Teodoro Nguema Obiang Mangue kwa kutumia nafasi yake ya uwaziri kufanya ubadhirifu wa utajiri wa taifa na kulipia gharama za maisha ya ufahari Marekani na kwingineko
Inaelekea kuna harakati madhubuti za kimataifa kuzikamata mali za Bwana Obiang.
Magari ya kifahari
Mwezi uliopita Ufaransa iliyakamata magari 11 ya kifahari na serikali ya Hispania ilikamata mali katika Madrid na visiwa vya Canary.
Mali zinazozuiliwa nchini Marekani ni pamoja na jumba la kifahari lililopo California, ndege ya muundo wa Gulfstream jet, gari ya muundo wa Ferrari yenye thamani ya zaidi ya dola nusu millioni na kumbukumbu za Michael Jackson .
Hati za mahakama zinaonyesha kumbukumbu hizi za Michael Jackson ni pamoja tuzo za uwanamuziki, tungo zake na jozi ya soksi ziliorembeshwa vito.
Habari za kusikitisha
Uchunguzi wa baraza la senet la Marekani mwaka 2004 kuhusu benki yenye makao yake Washington-Riggs Bank, uligundua familia ya Obiang iliitumia benki hiyo kupitisha pesa kutoka makampuni makubwa ya mafuta kama Exxon Mobil na wakati mmoja zaidi ya dolla millioni moja zililetwa katika benki zikiwa zimefungiwa katika karatasi ya plastiki.
Yote haya yangekuwa kichekesho ingekua si habari za kusikitisha.
Manufaa yao
Bwana Obiang,ambae anajulikana kama Teodorin, inasemekana alinufaika kutokana na hongo kama mwana wa Rais na waziri wa misitu. Equatorial Guinea iligundua mafuta katika miaka ya 1990 lakini imetajwa kama mfano wa laana ya kuwa na mali au kitendawili cha kuwa na mengi..
Vikundi vya kutetea haki za binaadamu vinaishtumu familia ya Obiang kwa kuinyonya nchi kwa manufaa yao wenyewe.
Asilimia 70 ya wakaazi wanaishi maisha ya ufukara na zaidi ya nusu nzima hawapati maji safi.
Kifungo
Ilikua katika juhudi za kumega sehemu ya utajiri wa mafuta wa nchi hiyo ndio kulizuka njama ya kile kilichojulikana kama mapinduzi ya Wonga mnamo mwaka 2004.
Askari mamluki Muingereza Simon Mann alikamatwa na kufungwa katika jela ya Black Beach lakini alichiliwa miezi 15 baadae kutoka kifungo cha miaka 34.
Aliwataja watu wengine mashuhuri akiwemo Mark Thatcher, mwana wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Margret Thatcher.
No comments:
Post a Comment