PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Sunday, 21 August 2011


Mwongozo Katiba mpya watolewa

20th August 2011
Chapa
Maoni
Jukwaa la Katiba Tanzania limezindua ‘Mwongozo wa Katiba kwa Raia’ unaopendekeza mjadala wa kupata Katiba mpya, kutosahau masuala 10 ya msingi, ikiwamo mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na Tanganyika kutambuliwa kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Masuala mengine ya kujadiliwa ni maadili ya taifa la Tanzania; mamlaka na madaraka ya Rais kuwa makubwa mno; na wabunge kutokuwa mawaziri na wakuu wa mikoa.
Pia muundo wa utawala wa nchi (mikoa, wilaya na halmashauri, kutokana na kuwapo mawazo kwamba, hakuna haja ya kuwa na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kuwa watendaji na wawakilishi wa wananchi katika halmashauri wanaweza kutosheleza kufanya majukumu ya kimaendeleo na kiutawala.
Mengine ni Muungano na hasa muundo wake; suala la kuwapo au kutokuwapo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ); adhabu ya kifo; na usawa halisi wa kijinsia (50:50).
Mwongozo huo, ambao ni mahsusi katika kuelezea kwa ufundi na wepesi utaratibu, mchakato na masuala muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa kuandika katiba ya kidemokrasia nchini, ulizinduliwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.
Kwa mujibu wa Kibamba, uchapishaji wa mwongozo huo, ambao uko katika mfumo wa kitabu, umegharimiwa na jukwaa hilo na kuhaririwa na Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Chris Maina Peter.
Alisema mwongozo huo unatoa historia ya Katiba ya sasa, mambo yaliyojiri na kusukuma upatikanaji wa katiba zote tano za nchi tangu uhuru (Tanganyika na Zanzibar) pamoja na kupendekeza namna bora ya kuendesha mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.
Mwongozo huu ni kiongozi cha namna tutakavyoweza kuandika Katiba ya wananchi wote wa Tanzania, hatua moja hadi nyingine,” alisema Kibamba.
Alisema maswali mengi, ambayo Watanzania wamekuwa wakijiuliza juu ya mchakato wa Katiba, yana majibu yake katika mwongozo huo.
Kibamba alisema mwongozo huo utasambazwa nchini kote kwa matumizi na kwamba, hakiuzwi bali kinasambazwa bure.
Alisema nakala za kitabu hicho (Mwongozo) zinapatikana kwa nakala za usambazaji na katika tovuti.
Kibamba alisema watu wote watakaohitaji kupata kitabu hicho kwa matumizi yao, ofisi zao na mengineyo kuanzia sasa, mchakato utakapokamilika mwaka 2014, nakala zitaendelea kupatikana katika kila mkoa, bara na visiwani kupitia vituo watakavyoendelea kuvitangaza kila mara.
Alisema kwa kuanzia, kila ofisi ya Jukwaa la Katiba Tanzania mikoani na wilayani, itakuwa na nakala za kutosha.
Kibamba alisema wana mpango kuchapisha nakala milioni moja, lakini kwa sasa wameanza na nakala 20,000 kwa gharama ndogo, ambazo hata hivyo, hakuzitaja.
Kazi nyingi serikalini zinaongezwa bei kwa mbinu za kifisadi. Tutachapisha nakala zozote zitakazohitajika hata kama ni zaidi ya milioni,” alisema Kibamba.
Aliongeza: “Ni matumaini yetu kuwa tutapata maoni, mapendekezo na ushauri juu ya namna mwongozo huu utakavyopokewa na jinsi ya urahisi au changamoto za utumiaji wake,” alisema Kibamba.
Alisema watakuwa tayari na wepesi wa kufanyia kazi mapendekezo yote yatakayowafikia kuhusiana na maudhui au upatikanaji wa chapisho hilo, lengo likiwa ni kufanikisha uongezaji wa kiwango cha uelewa na ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba nchini.

No comments:

Post a Comment