Tuesday, 30 August 2011

WADAU USOMENI KWA UMAKINI, HUU UPUPU MIMI UNANIWASHA SI JUI NYINYI

Mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika hatari ya kupoteza wanachama wake kama kitaendelea kukumbatia viongozi wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa za ufisadi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar, Raza alisema wakati umefika kwa Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi mazito ya kuwafukuza viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi ili kurejesha imani kwa wananchi na wanachama wa CCM kabla ya uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
“Viongozi wanaoshindwa kuzingatia maadili watimuliwe, haiwezekani mamilioni ya fedha yanaibiwa wakati huduma za jamii zikiendelea kuanguka nchini,” alisema Raza.
Hata hivyo, alisema juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Kikwete za kupambana na ufisadi zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wenzake ili lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania lifikiwe.
“Uongozi wake Rais Kikwete hivi sasa anateremka kilima, lakini tunaweza kupoteza na kupunguza wanachama kama watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi hawatachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola,” alisema Raza.
Alisema viongozi wengi wameshindwa kuheshimu misingi ya maadili ya uongozi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.
“Maadili waliyotuachia waasisi wa taifa hayapo tena Tanzania, kila mtu kawa mbabe sasa hatuna kiongozi katika nchi anayekemea maovu,” alisema Raza.
Alieleza kuwa rasilimali nyingi za nchi zinachukuliwa na kupotea huku Taifa likikabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na wanafunzi kuendelea kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.
Alisema ni jambo la kushangaza kwamba Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyokwapua mabilioni ya fedha, hadi sasa wahusika hawajachukuliwa hatua zozote za kisheria.
Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. milioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisema wakati Watanzania Bara wakikabiliwa na tatizo sugu la mgawo wa umeme, Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua hadi sasa viongozi wanaohusishwa na vitendo vya ufisadi.
Alisema wahusika katika kashfa ya ununuzi ya rada na wizi wa fedha za EPA lazima wakamatwe ili kulinda misingi ya sheria na utawala bora nchini.
“Kiongozi ukipata tuhuma tu katika chama inatosha kujiuzulu, usisubiri hadi uingizwe hatiani na vyombo vya sheria,” alisema Raza.
Alisema viongozi wa Afrika lazima wajifunze kwa kuangalia mfano wa yaliyotokea Misri baada ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Hosni Mubarak, alivyopelekwa mahakamani baada ya kuondolewa madarakani akiwa katika machela.
“Tumeona mfano Misri, aliyekuwa Rais kapelekwa mahakamani akiwa kabebwa katika machela … ndio maana nasema mafisadi wachukuliwe hatua kabla ya kulifikisha taifa pabaya,” alisema.
Alisema iwapo rasilimali za nchi zingesimamiwa vizuri na serikali, leo watoto wasingesoma wakiwa chini wala wananchi kukosa dawa katika hospitali na vituo vya afya pamoja na kutembea masafa marefu kusaka maji safi.
“Leo tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, watoto wetu wanasoma wakiwa wamekaa chini, hospitali zetu zina uhaba wa dawa, yote haya ni kukosekana kwa maadili ya uongozi,” alisema Raza.
Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, alisema marekebisho ya katiba mpya yafanyike kwa umakini mkubwa ili kuendeleza umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.
Alisema ni vizuri wananchi wakapewa uhuru wa kutosha kujadili na kuamua muundo wa Muungano wanaoutaka.
Hata hivyo, alisema kwamba Tume ya Katiba Mpya hakuna sababu ya kupangiwa zaidi ya miaka miwili kwa vile suala hilo linaweza kukamilika ndani ya miezi sita iwapo nia njema itakuwepo katika mabadiliko ya katiba.
Alipendekeza kuwa wabunge na wawakilishi wapewe uhuru wa kutosha wa kuamua wananchi wanataka Muungano wa aina gani na wajiepushe na kauli ambazo zinaweza kuibua matatizo wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya.
Raza ambaye aliwahi kuwa Mshauri wa mambo ya Michezo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, alisema Wazanzibari sio kunguru wala ndege ndani ya Muungano na kuwataka wabunge kuzingatia misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar badala ya kutoa kauli ambazo hazisaidii kujenga umoja wa kitaifa.
Kwa mujibu wa Raza, Wazanzibari wanaunga mkono Muungano, lakini uwe na maslahi ya kiuchumi kwa pande 

Polisi wapambana na wafuasi wa Malema

Julius Malema
Polisi wa Afrika Kusini wametumia magrunedi ya kushtua watu wanaomuunga mkono kiongozi Vijana wa ANC mwenye ushawishi Julius Malema wakati kamati ya maadili ya chama hicho ikimuhoji.
Bw Malema mwenye umri wa miaka 30, anatuhumiwa kwa ‘kusababisha mgawanyiko’ katika chama na kuleta kukiletea sifa mbaya alipotaka serikali ya Botswana ipinduliwe.
Awali akiwa mshirika wa karibu wa Rais Jacob Zuma, Bw Malema amekuwa akimkosoa zaidi Rais huyo.
Watu wanaomuunga mkono waliwarushia mawe polisi ambao walikuwa wakiwazuia mjini Johannesburg.
Polisi wameweka vizuizi vya vyuma na nyaya kufunga mtaa unaoingia jengo la Luthuli House, yaliko makao makuu ya ANC mahali kikao hicho kinafanyika.
Mamia ya watu wanaomuunga mkono Bw Malema wako nje, wakiimba na kuchoma moto takataka.
Wengine walichoma moto fulana yenye picha ya Rais Zuma, huku wengine wakiimba ‘Zuma lazima aondoke.’
Bw Malema, ambaye ameshtakiwa kwenye Tume pamoja na viongozi wengine watano wa vijana anaweza kufukuzwa kwenye chama katika kikao siri kinachoendelea.
Aliwekwa kwenye majaribio na Kamati ya Maadili mwaka jana baada ya kukutwa na makosa ya kumkosoa Bw Zuma.
Bw Malema, akiwa bado anachunguzwa kwa kuhusu tuhuma za ufisadi na rushwa, amesema atakubali uamuzi wa kamati hiyo.
"Tunawajibika kwa matendo yetu na tuko tayari kwa chochote. Tumekuwa tukisema siku zote kuwa ANC ndiyo hatima yetu, ikiwa hatima yetu itaondolewa basin a iwe hivyo," alisema.

Julius Malema ni nani?

Julius Malema, kiongozi wa Vijana wa ANC
  • Alizaliwa 1981, alijiunga na ANC akiwa na miaka 9
  • Alipata mafunzo ya kijeshi miaka ya 1990
  • 2008:alichaguliwa kiongozi wa Vijana wa ANC
  • 2008: aliapa ‘kuua’ kwa ajili ya Jacob Zuma
  • 2009: asema mwanamke ambaye Zuma alituhumiwa kumbaka ‘alifurahia kuwa naye’ –baadaye aliadhibiwa
  • Akatoa wito kwa migodi itaifishwe na mashamba yanayomilikiwa na wazungu yachukuliwe.
  • 2010: alizdhibiwa kwa kumdharau Zuma
  • 2011: alihukumiwa kwa kuimba "Ua kaburu [Wakulima wa kizungu]"
  • Alitoa wito serikali ya Botswana ipinduliwe
  • Alituhumiwa kwa kuishi maisha kifahari

Kauli za utata

Mwandishi wa BBC anasema kiongozi huyo wa Vijana ametoa wito sekta ya madini itaifishwe na kwamba umiliki wa mashamba ya wazungu una ubia na viongozi wa chama hali ambayo imempa umaarufu zaidi wa kisiasa katika jamii ya weusi wanaokabiliwa na ufukara.
Mwandishi wa BBC Karen Allen amemwelezea Bw Malema kuwa ni ‘mwenye ushawishi mkubwa kwa viongozi na mwanasiasa’ ambaye kundi lake la vijana linailetea ANC kura 350,000 na ushawishi kwa viongozi waandamizi wa anc wanaotaka kupandishwa vyeo.
Hatua za kinidhamu dhidi yake zitaleta picha ya mbio za uchaguzi wa chama hicho mwakani.
Nia ya Bw Zuma kutaka kipidni cha pili cha Urais wa ANC itakuwa na nguvu iwapo umaarufu wa Bw Malema utatupiliwa mbali, mwandishi wa BBC anasema.
Iwapo, itakavyokuwa, kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa atatoka kwenye kikao hicho akiwa na uanachama wake, Rais Zuma atakabiliwa na hatima isiyotabirika, anasema.
Kwa muda mrefu kiongozi huyo wa vijana amekuwa mwenye utata.
Alikuwa mtu muhimu aliyemsaidia Bw Zuma kuchukua udhibiti wa ANC kutoka kwa mtangulizi wake Thabo Mbeki mwaka 2008 akampigia kampeni kali katika uchaguzi wa 2009 ambao ulimweka madarakani Bw Zuma.
Lakini Jumatatu, alisema hakuwa na uhusiano wowote binafsi na Rais isipokuwa wa kikazi.
Mwezi Mei 2010, alilazimishwa kuomba radhi hadharani kufuatia safari yake Zimbabwe iliyokuwa na utata ambako alitangaza kwamba ANC inamuunga mkono Rais Robert Mugabe wakati Bw Zuma alikuwa mpatanishi wa mgogoro wa serikali ya muungano nchini Zimbabwe.
Bw Malema aliadhibiwa na ANC kwa kumfukuza mwandishi wa BBC kwenye mkutano waandishi wa habari na kutotii amri za chama kwa kukataa kuacha kuimba wimbo maarufu uliokuwa na ushawishi wakati wa ubaguzi wa rangi ‘Ua kaburu[mkulima mzungu]

Monday, 29 August 2011

MWANA MAMA SHUJAA WA AFRICA,


Unamfahamu Oprah Winfrey?

Oprah Winfrey, Rais Obama na mkewe Michelle
Moja ya vipindi vinavyotazamwa sana katika historia ya Marekani, The Oprah Winfrey Show, kinamalizika baada ya miaka 25. Kipindi chake kimegusa wengi na kuvuka mipaka ya televisheni.
Kipindi chake cha kwanza, kilichoitwa Namna ya Kumwoa au Kuolewa na mtu wa Chaguo lako, kilipendekezwa kiwe kipindi kinachorushwa mchana kama kipindi chengine chochote cha kawaida.
Lakini baada ya vipindi 4,560, watu maarufu kama Madonna, Beyonce na Tom Hanks wanatarajiwa kutokea kwenye kipindi chake cha mwisho cha kuagwa, kinachorushwa hewani siku ya Jumatano.
Wakati wa miaka hiyo 25, Winfrey limekuwa jina maarufu sana, anayekubalika na wengi na ni mmoja wa matajiri katika ulimwengu huu.
Akimaliza na kuendelea kufanya kazi katika televisheni yake mwenyewe, uwezo wa kupata wageni wanaovutia kwenye habari haliwezi kudharauliwa.
Mwezi huu, Rais Obama alizungumzia kwanini alihitaji kutoa cheti chake cha kuzaliwa hadharani.
Na Sarah Ferguson alizungumzia kwanini hakualikwa kwenye harusi ya kifalme Uingereza.
Kwahiyo ni namna gani ambavyo Winfrey ameweza kufanikiwa? Mambo 10 yanajumuisha ushawishi wake.

ATOA MADAI YA KUDHALILISHWA KIJINSIA, 1986

Oprah Winfrey
Katika hatua yake ya kukiri ambapo baadae ikaja kuwa namna ambavyo anafanya kazi, Oprah aliwaambia watazamaji wake kuwa alibakwa alivyokuwa mtoto.
Si kwamba tu ilisababisha mwanzo wa kampeni isiyo rasmi kuhusu udhalilishaji, iliweka njia kwa msururu wa watu-maarufu wenye mtawaliwa, watu wa kawaida wenye mambo ya kueleza- kukaa kwenye kochi lake na kukiri.
Mwandishi wa vitabu Bonnie Greer, aliyeondoka kwao Chicago mwaka huo huo ambao Oprah alianza kupanda chati mjini humo, alisema: " Amefanya mawazo yaliyo ya wengi yakubalike kirahisi lakini anaielezea kama inamhusu moja kwa moja mwanamke wa Kimarekani mweusi.
"Imekuwepo siku nyingi katika utamaduni wa Kimarekani, lakini Oprah aliileta kwenye televisheni wakati wa mchana. Alianzisha utamaduni wa "mwathirika" kwa mantiki ya uzuri na ubaya.
"Aliingia wakati wa msukosuko wa uchumi katikam iaka ya mwisho ya 80 na mwanzo wa 90, jambo ambalo Wamarekani walitaka kuhakikishiwa: namna ya kuhimili na uzuri wetu.
"Oprah alizungumzia vitu kwa waliokuwa wakitazama vipindi vyake kwasababu alitaka kuonyesha 'uzuri' na 'uaminifu' yana malipo yake hapa duniani.

MKOKOTENI WA MAFUTA, 1988

Akiwa amevaa jeans ya saizi 10, Winfrey aliyekuwa mwembamba aliingia kwenye jukwaa wakati wa kipindi chake na mkokoteni wa mafuta kuonyesha namna alivyopoteza kilo 30 kwa kipindi cha miezi minne kwa kutokula kitu zaidi ya Optifast.
Lakini uzito ukaanza kurudi na ikawa mwanzo wa miongo miwili ya kupunguza kiwango cha kula na kupambana ili kukifanya kiuno kiwe kidogo.
Tim Teeman, mwandishi wa Marekani wa gazeti la Times, alisema: " Ikiwa Oprah atakumbukwa kwa lolote, basi ni umbo lake."
"Unaweza kusema haitoi ujumbe wa kweli lakini unatoa ujumbe sahihi. Jinsi Oprah alivyozungumzia uzito ni hali halisi ya namna watu mbalimbali wanavyopambana na uzito wao.

MICHAEL JACKSON ATOBOA, 1993

Idadi kubwa ya waliokuwa wakiangalia kipindi cha Winfrey illiongezeka alipomhoji Michael Jackson wakati umaarufu wake ulipozidi kupamba moto.
Takriban watazamaji milioni 62 walimwona ndani ya Neverland mtu aliyenaswa kwenye utoto wake, kabla ya madai ya kudhalilisha watoto kuibuka na kumharibia sifa yake.
Wakati wa mahojiano yaliyochukua dakika 90, alimwambia alikuwa akiumwa maradhi ya ngozi na alikana kuwa alilala kwenye chumba chenye gesi ya oksijeni.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michael kuzungumza kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka mingi na ilionekana kuwa jambo la kipekee kwa kipindi cha Winfrey, na kuandikwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali duniani na kusaidia kuimarisha sifa yake.

ELEN DEGENERES AJITOA HADHARANI, 1997

Mchekeshaji wa Marekani, mwendesha kipindi kwenye televisheni na muigizaji Ellen DeGeneres alisema hadharani kuwa anafuata mapenzi ya jinsia moja kwenye kipindi hicho.
Mahojiano hayo yalifungua mlango upya kwa kazi ya DeGeneres ambaye alianzisha kipindi chake mwenyewe cha mahojiano.
Mvuto wa Winfrey kwa wanawake wengine umejadiliwa sana.
Greer alisema, " Ni mtetezi wa wanawake kwa minajil ya kwamba amejenga milki yake mwenyewe na mfano wake umesababisha wanawake wengine kuiga."
"Ni wazi kwa hakika anakupa msukumo, hodari sana na mwerevu na amefanya mambo mazuri. Kila mmoja anamtakia kheri, pamoja na mimi.
Licha ya kukiri kuhusu masuala yake ya uzito na udhalilishaji, na uwezo wake wa kufanya wengine kama DeGeneres kuwa wazi, inashangaza namna ambavyo tunajua machache kuhusu Winfrey mwenyewe, alisema Greer.
" Kila mmoja aliye karibu yake hazungumzii mambo yake. Ni miongoni mwa watu maarufu Marekani ambao tunajua kila kitu na hatujui kitu vile vile.

TOM CRUISE JUU YA KOCHI, 2005

Huenda wakati utakaokumbukwa zaidi kwa Oprah ni pale Tom Cruise alipoanza kuchekacheka, akiruka juu na chini kwenye kochi lake alipoelezea penzi lake kwa mpenzi wake mpya, Katie Holmes, ambaye kwa sasa ni mke wake.
Teeman alisema tangu wakati huo tendo lake hilo limekuwa likifanyiwa dhihaka na kuigwa kwa kubezwa. Huu ni wakati ulioainisha kazi yake, baada ya filamu kama Top Gun, Cocktail au Mission Impossible.
"Oprah alionekana kumahanika, akifikiria 'Anafanya nini?' Kazi yake iliporomoka kwa muda lakini amerudi."
Watu maarufu hushiriki kipindi cha Oprah kuondosha pepo mbaya au kukiri jambo la kimapenzi, alisema, na wanajua hatowapa wakati mgumu.

JAMES FREY ALAANIWA, 2006

Moja ya ushawishi mkubwa aliokuwa nao Winfrey umekuwa katika ulimwengu wa uchapishaji vitabu, klabu yake ya vitabu imekuwa kisifiwa kwa kutengeneza mamilioni kwa waandishi ambao vitabu vyao hujadiliwa kwenye klabu yake.
Hakuna pahala ambapo ushawishi wake ulionekana kama katika kesi ya James Frey. Kitabu chake cha A Million Little Pieces, iliyoelezea hadithi yake ya kujikwamua kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, ambapo ilikuwa kitabu kilichouzwa kwa kiwango kikubwa baada ya kutokea kwenye kipindi chake.
Lakini mwaka 2006, baada ya kuwa na shaka na maisha yake aliyoyaeleza Frey, Winfrey alimwalika tena mwandishi huyo ili kumhoji, iliyosababisha mabishano makali na kuvua nguo hadharani kwa Frey.
Licha ya Winfrey kuelezea hivi karibuni kujuta kwa namna alivyolishughulikia suala hilo, alichojifunza si kukereka, alisema Teeman.
Kipindi chake ni kuhusu nia njema, na kitendo cha kusaliti uaminifu huo ni kuaibika.

SHULE YA AFRIKA KUSINI YAFUNGULIWA, 2007

Oprah na wanafunzi Afrika Kusini
Shule ya uongozi ya Winfrey, karibu na Johannesburg, ilifunguliwa mwaka 2007 kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 40.
Aliahidi kujenga shule hiyo baada ya kukutana na aliyekuwa rais wa Afrika kusini Nelson Mandela mwaka 2002.
Winfrey mwenyewe aliwahoji wasichana wengi wa Afrika kusini waliotoka kwenye familia maskini walioomba nafasi 150 za mwanzo katika shule hiyo.
Mwaka jana, aliyekuwa matroni wa chuo hicho alifutiwa mashtaka ya kudhalilisha mabinti chuoni hapo.
Winfrey alieleza namna alivyosikitishwa wakati hukumu ilipotolewa lakini alisema anajivunia kwa namna wasichana hao walivyopata ujasiri wa kutoa ushahidi.
Ufadhili wake unajulikana, na wakfu wake wa Oprah Winfrey umechangia mamilioni ya dola kwa miradi Marekani na nchi za nje, huku shirika lake la ihsani Oprah's Angel limechanga kiasi cha dola za kimarekani milioni 80.

BARACK OBAMA, SI CLINTON, 2007

Katika mkutano Iowa mwaka 2007, Oprah Winfrey alimwuunga mkono Barack Obama ambaye kwa wakati huo alikuwa akigombea nafasi ya urais kupitia chama cha Democrat na Hillary Clinton.
Kuunga mkono kwake Winfrey kulionekana kuwa muhimu sana katika mpambano wa karibu wa nafasi hiyo kutokana na ushawishi mkubwa alionayo. Lakini chaguo lake liliacha maswali mengi.
" Alipomwuunga mkono Obama kwa nafasi ya urais watazamaji wake, ambao ni wanawake wazungu wa makamo, walikuwa wakimwuunga mkono Hillary Clinton na akakuta wengi wakimwacha mkono kwa kudhani anachagua asili au jamii yake kuliko jinsia yake. Alisema Eric Deggans, mkosoaji kupitia televisheni ya Petersburg Times huko Florida.
Umaarufu wake mkubwa ulitikisika kwenye jamii ya watu weusi alipokosoa muziki wa miondoko ya rap kwa mashairi yaliyo na chuki kwa wanawake.
Mara zote amekuwa akijiwakilisha kama mweusi lakini si kiais hicho cha kuwapoteza watazamaji walio wengi, alisema Deggens.
Lakini Winfrey ameonyesha, kama alivyofanya Bill Cosby kabla yake na Barack Obama baadae, kinachowezekana kwa Mmarekani mweusi.
"Kwa kufikia kiwango hicho kwenye televisheni, Oprah ameonyesha unaweza ukang'ara kama mtu mweusi.
"Amekuwa sauti ya wanawake weupe wa makamo kwa namna ambavyo haijawahi kufanywa na mtu yeyote, na kwa watu weusi kuona Mmarekani mweusi anakubalika kwa moyo mmoja ni muhimu sana."

KUAGWA NA WATU MAARUFU, 2011

Tom Hanks akimuaga Oprah
Moja ya vipindi vya mwisho vya Oprah Winfrey huko Chicago uligeuka kuwa usiku uliojaa machozi, shukrani na watu mashuhuri kama vile Tom Cruise, Will Smith na Madonna.
" Jambo kuhusu Oprah ambalo linapendeza ni kwamba ameweza kuunda alama inayojumuisha utata mkubwa.
" Ni rafiki yako halisi ambao marafiki zake ni Julia Roberts na Tom Cruise. Ni kiongozi wa dini anayefanya kazi kupita kiasi na hufanya kipindi kwa mwaka kuhusu vitu vyote vya gharama anavyopenda.
"Ni kiongozi wa dini asiyechagua kanisa lipi aende. Ni mwanamke anayeteta wazazi wa kike na desturi za kifamilia lakini binfasi hana watoto."
Utata huu unavutia wanawake, alisema." Wanashukuru kwamba wanaweza kumwangalia Oprah na kuona mtu kama rafiki yao wa karibu lakini pia huwapa nafasi katika ulimwengu huu mzuri.

Maporomoko Uganda yaua watu Bulambuli

Maporomoko yatokea tena baada ya yaliyotokea mwaka 2010
Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wanasema.
Wakazi wanahofu kuwa 35 huenda wamekufa katika wilaya ya Bulambuli lakini mpaka sasa miili 24 imepatikana.
Mwaka uliopita mamia walikufa katika tukio kama hilo katika miteremko ya Mlima Elgon.
Maafisa wanasema watawahamisha hadi nusu milioni ya watu kuepuka hali hiyo kujitokeza tena.
Waliokufa Bulambuli, kilometa 270 (maili 167) kaskazini mashariki mwa Kampala, wanatokea kwenye vijiji viwili, mseamji wa Shirika la Msalaba Mwekundu Catherine Ntabadde ameliambia shirika la habari la AFP..
Amesema watu wawili wameokolewa.
Kufuatia janga la Mlima Elgon, imearifiwa kuwa ongezeko la watu la haraka limesababisha kukatwa kwa miti kwenye milima na kufanya maporomoko na mafuriko kutokea mara kwa mara.

Kanali Gaddafi 'bado tishio' Libya

Waasi Libya
Mkuu wa waasi nchini Libya amesema, Kanali Muammar Gaddafi bado ni tishio nchini humo na duniani kwa ujumla.
Mkuu wa Baraza la mpito la taifa (NTC) Mustafa Abdul Jalil alisema majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato, na washirika wengine lazima waendelee kuwaunga mkono waasi dhidi ya 'mtawala wa mabavu.'
Waasi wameudhibiti mji mdogo wa Nofilia wakielekea kwenye ngome ya Kanali Gaddafi- na mji alipozaliwa-Sirte.
Hadi sasa haijulikani Kanali Gaddafi alipo tangu waasi walipoingia Tripoli wiki iliyopita, na kuteka makazi yake.
Tayari wanadhibiti eneo kubya ya Libya, baada ya mapigano yaliyodumu kwa miezi kadhaa tangu maandamano yalipoanza.
Akizungumza katika mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi huko Qatar, mkuu wa NTC, Mustafa Abdul Jalil, alisema majeshi ya Kanali Gaddafi bado yanaweza kujibu mashambulizi hata baada ya waasi kupambana dakika za mwisho na majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi.
Waasi wanasema wako katika mazungumzo na viongozi wa kikabila wa Sirte ili kuzuia umwagikaji damu, lakini mpaka sasa hawajafanikiwa.
Mwandishi wa BBC Paul Wood ambaye yupo na waasi wakielekea Sirte alisema, huenda ikawa bado viongozi wa kikabila wanayo akilini onyo alilotangaza Kanali Gaddafi kuwa waasi wanaingia mjini humo kupora na kubaka wanawake.
Huku majeshi ya kivita yakiendelea kuwaunga mkono waasi, waasi wanatarajiwa kupigana kwa kile kinachoonekana kuwa makali ya mwisho ya vita hivi na kwa ajili ya mapinduzi yao.
Azimio la Nato linaendelea mpaka mwisho wa Septemba ambapo itabidi ipitiwe upya na nchi wanachama wote.

SAMAHANI KWA WADAU

kuna baadhi ya picha niki post, baada ya muda zinatoka hili swala lipo nnje ya uwezo wangu ila nalifanyia kazi, na nikigundua picha imetoka huwa nai delete halaka sana maana isichafue uwanja wetu.

Sunday, 28 August 2011


Man U yaifanyia mauaji Arsenal 8-2



Wayne Rooney amepachika mabao matatu peke yake wakati Manchester United ikiinyuka Arsenal kwa mabao 8-2.
Young
Young na Rooney

Danny Welbeck ndiye alifungua karamu ya magoli baada ya kuunganisha pasi ya Anderson.
David De Gea aliokoa penati iliyopigwa na Robin Van Persi, na baadaye kidogo Ashely Young kufunga bao la pili.
Rooney aliandika bao la tatu na la nne kwa mikwaju miwili ya adhabu, kabla ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati.
Nani na Park Ji Sung walifunga nao na Ashley Young kuongeza jingine.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Robin Van Persie.
Awali Manchester City waliizaba Tottenham Hotspur kwa mabao 5-1.
Edin Dzeko alifunga mabao manne, na Sergio Aguero akifunga moja. Bao pekee la Spurs lilifungwa na Younis Kaboul.
Kwingineko Newcastle United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham. Leon Best akifunga mabao yote ya Newcastle na goli la Fulham kufungwa na Clint Dempsey.
West Brom walishindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Stoke City. Goli hilo pekee lilifungwa na beki Ryan Shotton katika dakika ya 89.

Wapiganaji wa Libya wakataa mazungumzo

Wapiganaji wa Libya wanasema hawataki kufanya majadiliano na Kanali Gaddafi, baada ya pendekezo hilo kutolewa na msemaji wa kanali.
Wapiganaji wakiwa Ras Lanuf, kabla ya kusonga Sirte
Na wapiganaji wa Libya piya wamesema wana wasiwasi juu ya usalama wa watu kama elfu 50, waliokamatwa na jeshi la Kanali Gaddafi katika miezi ya karibuni.
Wanafikiri watu hao wamezuwiliwa kwenye mahandaki mjini Tripoli, na wamewaomba watu wanaojua mahandaki hayo yaliko, wawape taarifa.
Piya wanasema shehena za mafuta na maji zinaanza kuwasili Tripoli leo, na meli zenye shehena za maji na mafuta ya vinu vya umeme, zinatarajiwa kutia nanga katika siku mbili tatu zijazo.
Kanali Gaddafi bado hajulikani aliko, lakini mtu anayefikiriwa kuwa msemaji wake, amelipigia simu shirika la habari New York, kusema Gaddafi yuko tayari kujadiliana na upinzani, ili kuunda serikali ya mpito.
Msemaji wa wapiganaji alieleza kuwa mto ambao ndio unaipatia Tripoli maji, umetiwa sumu na jeshi la Gaddafi, kwa hivo umefungwa.
Katika ghala moja ya Tripoli, waandishi wa habari wamekuta maiti zilizoteketea za wanaume 50.
Inavoelekea waliuliwa na jeshi la Gaddafi, lilipokuwa likikimbia.
Shirika la habari la AP mjini New York, linasema limepigiwa simu na mtu waliyemtabua kuwa msemaji wa Kanli Gaddafi, Moussa Ibrahim, ambaye amejificha Libya.
Alisema kuwa Gaddafi sasa yuko tayari kujadili serikali ya mpito, na mazungumzo hayo yaongozwe na mwanawe, Saadi.
Lakini kama Gaddafi mwenyewe hatosallim amri, pendekezo hilo litaonekana kuwa Gaddafi bado anjidanganya.


Mbu wa malaria wamepungua Afrika


Wanasayansi wanasema mbu wanaoambukiza malaria wanaadimika katika sehemu za Afrika, lakini hawajui sababu.
Mtoto anaugua malaria Afrika

Data kutoka nchi kama Tanzania, Eritrea, Rwanda, Kenya na Zambia inaonesha malaria inapungua haraka ; labda kwa sababu ya miradi kama ile ya kutumia vyandarua venye dawa.
Lakini wanasayansi wa Tanzania na Denmark wanasema hata mitego yao inanasa mbu wachache, kutoka elfu 5 mwaka wa 2004 na kushuka hadi mbu 14 mwaka wa 2009.
Mitego hiyo iko katika vijiji visivokuwa na vyandarua vya dawa.
Sababu inaweza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa..kwamba misimu ya mvua imebadilika na hivo kuchafua msimu wa uzazi wa mbu.
Lakini aliyeongoza utafiti huo, Professor Dan Meyrowitsch, hakubaliani na hayo, anafikiri sababu hasa ni kuwa pengine kuna ugonjwa uliotapakaa kati ya mbu na kuwafyeka wengi, au mabadiliko katika mazingira yao ambayo hayawafai

Usilale...


Mahakama moja nchini Malaysia imemhukumu kwenda jela miaka mitano mwizi mmoja aliyekutwa kalala katika nyumba aliyovunja kwenda kufanya wizi.
Lala
Usilale ukiwa 'kazini'..

Mtandao wa habari wa Canadian press umemkariri mwendesha mashitaka Mohammad Ashraff Diah akisema mwizi huyo alivunja nyumba moja kusini mwa Malaysia wiki iliyopita na kujilaza kitandani na kupitiwa na usingizi fofofo.
Mwenye nyumba hiyo aliporejea asubuhi alimkuta mwizi huyo bado kalala, na kuamua kuita polisi kabla ya mwizi huyo kuamka. Mwizi huyo alikurupuka baada ya polisi kuwasili, na kujaribu kukimbia. Mwizi huyo alikamatwa na dola kadhaa alizokuwa ameimba katika nyumba hiyo. Mwendehsa mashikata Ashraff amesema juzi Jumatano kuwa mwizi huyo alikiri makosa ya wizi, ingawa hakusema lolote kuhusu suala la kulala..

Afande mabawa

Jeshi la Uchina limetangaza kutoa ajira kwa njiwa elfu kumi.
Njiwa
Njiwa akibebeshwa ujumbe

Njiwa hao wameajiriwa ili waweze kutimika kwa ajili ya mawasiliano, iwapo itatokea siku ambayo njia za kawaida za mawasiliano zitaharibika, au kukwama. Kituo cha televisheni cha Uchina CCTV kimesema ajira hiyo imetolewa na Jeshi la Ukombozi la watu wa China.
Taarifa zinasema tayarinjiwa hao wameanza kupewa mafunzo, katika jiji moja katikati ya Uchina.
Njiwa
Afande..
Jeshi hilo la njiwa litatumika katika siku ambayo mawasiliano yataharibika, na kazi yao itakuwa kuwasilisha ujumbe muhimu. Maafande hao wenye mabawa pia watakuwa wakipewa kazi nyeti za kijeshi. Njiwa wamekuwa wakifanya kazi katika jeshi la Uchina tangu miaka ya hamsini, ingawa sio kwa kiasi kikubwa kama hawa walioajiriwa sasa.

Majina hayo...

Nchini Misri, bwana mmoja ameamua kumuita mwanae wa kike "Facebook" ili kuenzi mtandao huo wa kijamii uliosaidia kumuondoa rais Hosni Mubarak wa nchi hiyo.
Facebook
Facebook

Gazeti la Al-Ahram limeripoti siku ya Jumatatu kuwa wbana huyo Jamal Ibrahim, alimpa jina hilo mwanaye huyo wa kwanza kuonesha furaha yake na kufikia malengo ya waandamanaji nchini Misri.
Maelfu ya vijana wa Misri walitumia mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na mingineyo kuandaa maandamano, yaliyosababisha kuondoka kwa rais Mubarak aliyetawala Misri kwa miaka thelathini. Facebook ina watumiaji milioni tano na mia tano nchini Misri.


Taratibu na majina


Bwana mmoja katika Falme za Kiarabu ameamua kubadili jina lake kuwa "Umoja" baada ya kuzuka vya vuguvugu la kisaisa katika nchi za Kiarabu hivi karibuni. Bwana huyo jina lake halisi ni Moamer Kadafi.
Gaddafi
Muammar Gaddafi

Gazeti la Emirati limesema bwana huyo raia wa Sudan anaishi katika mji wa Sharjah.
Gazeti hilo limesema Bwana Kadafi anabadili jina lake ili kuungana na waandamanaji wanaompiga kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi. Bwana huyo mwenye umri wa miaka arobaini amesema alipewa jina hilo na baba yake, mwaka mmoja baada ya kuzaliwa, ambapo Kanali Gaddafi aliingia madarakani.
"Nilikuwa najivunia sana jina hilo, na hata nilikuwa nikichana nywele kama Gaddafi" amesema Kadafi, ambaye huenda hivi karibuni ataanza kuitwa Umoja.
"Sasa hivi najisikia vibaya kuwa na jina hili" ameongeza raia huyo wa Sudan.

UKO WAPI UBINAADAM


Maiti zagundulika hospitalini Libya

Hospiatli ya Abu Salim mjini Tripoli
Miili iliyotelekezwa katika hospitali ya Abu Salim kufuatia mapigano
Zaidi ya miili ya watu 200 imepatikana katika hospitali iliyotelekezwa katika mji mkuu wa Libya Tripoli .
Mwandishi wa BBC ambaye alikwennda katika hospitali ya Abu Salim aliikuta miili ya wanaume ,wanawake na watoto kwenye vitanda na veranda na pia damu nyingi iliyotapakaa kwenye sakafu .
Madaktari na wauguzi walikuwa wameitoroka hospitali hiyo kufuatia mapigano.
Walionusurika wanasema wengi waliokuwa na majeraha waliachwa bila matibabu hadi kufa , huku wengine ikioza kando yao.
Katika mji mkuu wa Tripoli kuna taarifa kuhusu kupatikana kwa mamia ya miili ya watu waliouawa baadhi yao wakiwa wamekatwa mikono.
Pande mbili zinazohusika na mzozo nchini Libya zimekuwa zikilaumiwa kwa mauji hayo.

Kimbunga Irene kinavuma Marekani

Watu zaidi ya milioni mbili hawana umeme na kwa uchache wanane wamekufa wakati kimbunga Irene kilipopiga kanda ya mashariki ya Marekani.
Kimbunga Irene kama kinacoonekana kutoka anga za juu
Kimbunga hicho kimepungua kasi tangu kufika mwambao lakini hata hivo kinatarajiwa kuleta uharibifu mkubwa, hasa kwa sababu ya mafuriko.
Kimbunga hicho kiitwacho Irene kinafwata mkondo uliotabiriwa, kutoka kusini kuelekea kaskazini mwa kanda ya mashariki.
Kimeshamwaga mvua zaidi ya thuluthi ya mita katika sehemu fulani, na kuna ripoti kuwa mawimbi yamefumka kufika urefu wa karibu mita tatu.
Kinatarajiwa kupiga Philadelphia, Boston pamoja na mji wa New York, ambako wakaazi zaidi ya elfu 20 tayari wameshapoteza umeme kwa sababu ya upepo mkali.
Meya wa New York, Michael Bloomberg amefunga reli za chini kwa chini, na amewaomba wakaazi wasitoke nje hadi dhoruba ikishapita.
Wasiwasi mkubwa ni juu ya Mto Hudson usije ukajaa maji na kufurika katika mitaa ya Manhattan pamoja na Wall Street, mtaa wa masoko ya fedha.
Rais Obama amefupisha likizo yake ili kusimamia shughuli za serikali za kupambana na dhoruba hiyo.
Anataka kuepuka makosa yaliyofanywa wakati wa kimbunga Katrina, miaka 6 iliyopita, ambapo serikali ilichelewa kuchukua hatua.

Saturday, 27 August 2011


Vituo vya Polisi na Benki vyashambuliwa Nigeria

Shambulio la Boko haram Nigeria
Takriban watu 12 wameuawa katika shambulio kwenye benki mbili na vituo viwili vya polisi katia mji wa Gombi jimbo la Adamawa kaskazini mwa Nigeria.
Maafisa katika eneo hilo wanasema huenda kundi la Kiislam la Boko Haram limehusika na mashambulio hayo siku ya Alhamisi.
Polisi, wafanyakazi wa baenki na wateja wameuawa, huku waliofanya shambulio hilo wakikimbia na silaha na fedha, ripoti zinasema.
Boko Haram, liliundwa mwaka 2002, linapigania kuwepo utawala wa Kiislam nchini Nigeria.
Mkazi wa Gombi, Husseini Abdurrazak, alisema aliwaona watu wenye silaha wakivamia kituo cha polisi na kutoroka na silaha kabla ya kuiba kwenye benki, shirika la Habari la AFP limeripoti.
"Walikuwa wakiimba 'Allahu Akbar' na tunahisi huenda wanaweza kuwa wanachama wa Boko Haram au ni wezi tu wenye silaha waliojifichia kwenye kundi hilo," alisema.
Majadiliano
Mwandishi wa BBC Abdullahi Kaura Abubakar mjini Kaduna anasema mamlaka katika eneo hilo wanaamini huenda watu hao wenye silaha ni kutoka Boko Haram.
Kundi hilo limekubuhu kwa mashambulizi ya vituo vya polisi na mabenki kaskazini mwa Nigeria kuendesha harakati zake, mwandishi wetu anasema.
Miaka miwili iliyopita, vikosi vya usalama vya Nigeria kikatili vilizima kuinuka kwa kundi hilo, vikiharibu makazi yake mjini Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno na kisha kumshika na kumuua kiongozi wake Mohammed Yusuf.
Badala ya kutoweka, kundi hilo limeibuka tena mwezi Septemba mwaka jana na kuapa kulipiza kisasi kifo cha kiongozi wake.
Mwezi Juni, Boko Haram lilisema limefanya mashambulizi katika makao makuu ya polisi mjini Abuja na kuua watu sita.
Katika kujibu, vikosi vya usalama vimeanzisha harakati nyingine ya kulivunja kundi hilo wakati Rais Jonathan Goodluck ameteua kamati kufanya uchunguzi wa wazi na viongozi wake.