Tuesday, 30 August 2011

WADAU USOMENI KWA UMAKINI, HUU UPUPU MIMI UNANIWASHA SI JUI NYINYI

Mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika hatari ya kupoteza wanachama wake kama kitaendelea kukumbatia viongozi wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa za ufisadi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar, Raza alisema wakati umefika kwa Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi mazito ya kuwafukuza viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi ili kurejesha imani kwa wananchi na wanachama wa CCM kabla ya uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
“Viongozi wanaoshindwa kuzingatia maadili watimuliwe, haiwezekani mamilioni ya fedha yanaibiwa wakati huduma za jamii zikiendelea kuanguka nchini,” alisema Raza.
Hata hivyo, alisema juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Kikwete za kupambana na ufisadi zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wenzake ili lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania lifikiwe.
“Uongozi wake Rais Kikwete hivi sasa anateremka kilima, lakini tunaweza kupoteza na kupunguza wanachama kama watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi hawatachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola,” alisema Raza.
Alisema viongozi wengi wameshindwa kuheshimu misingi ya maadili ya uongozi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.
“Maadili waliyotuachia waasisi wa taifa hayapo tena Tanzania, kila mtu kawa mbabe sasa hatuna kiongozi katika nchi anayekemea maovu,” alisema Raza.
Alieleza kuwa rasilimali nyingi za nchi zinachukuliwa na kupotea huku Taifa likikabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na wanafunzi kuendelea kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.
Alisema ni jambo la kushangaza kwamba Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyokwapua mabilioni ya fedha, hadi sasa wahusika hawajachukuliwa hatua zozote za kisheria.
Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. milioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisema wakati Watanzania Bara wakikabiliwa na tatizo sugu la mgawo wa umeme, Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua hadi sasa viongozi wanaohusishwa na vitendo vya ufisadi.
Alisema wahusika katika kashfa ya ununuzi ya rada na wizi wa fedha za EPA lazima wakamatwe ili kulinda misingi ya sheria na utawala bora nchini.
“Kiongozi ukipata tuhuma tu katika chama inatosha kujiuzulu, usisubiri hadi uingizwe hatiani na vyombo vya sheria,” alisema Raza.
Alisema viongozi wa Afrika lazima wajifunze kwa kuangalia mfano wa yaliyotokea Misri baada ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Hosni Mubarak, alivyopelekwa mahakamani baada ya kuondolewa madarakani akiwa katika machela.
“Tumeona mfano Misri, aliyekuwa Rais kapelekwa mahakamani akiwa kabebwa katika machela … ndio maana nasema mafisadi wachukuliwe hatua kabla ya kulifikisha taifa pabaya,” alisema.
Alisema iwapo rasilimali za nchi zingesimamiwa vizuri na serikali, leo watoto wasingesoma wakiwa chini wala wananchi kukosa dawa katika hospitali na vituo vya afya pamoja na kutembea masafa marefu kusaka maji safi.
“Leo tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, watoto wetu wanasoma wakiwa wamekaa chini, hospitali zetu zina uhaba wa dawa, yote haya ni kukosekana kwa maadili ya uongozi,” alisema Raza.
Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, alisema marekebisho ya katiba mpya yafanyike kwa umakini mkubwa ili kuendeleza umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.
Alisema ni vizuri wananchi wakapewa uhuru wa kutosha kujadili na kuamua muundo wa Muungano wanaoutaka.
Hata hivyo, alisema kwamba Tume ya Katiba Mpya hakuna sababu ya kupangiwa zaidi ya miaka miwili kwa vile suala hilo linaweza kukamilika ndani ya miezi sita iwapo nia njema itakuwepo katika mabadiliko ya katiba.
Alipendekeza kuwa wabunge na wawakilishi wapewe uhuru wa kutosha wa kuamua wananchi wanataka Muungano wa aina gani na wajiepushe na kauli ambazo zinaweza kuibua matatizo wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya.
Raza ambaye aliwahi kuwa Mshauri wa mambo ya Michezo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, alisema Wazanzibari sio kunguru wala ndege ndani ya Muungano na kuwataka wabunge kuzingatia misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar badala ya kutoa kauli ambazo hazisaidii kujenga umoja wa kitaifa.
Kwa mujibu wa Raza, Wazanzibari wanaunga mkono Muungano, lakini uwe na maslahi ya kiuchumi kwa pande 

No comments:

Post a Comment