Tuesday, 30 August 2011


Polisi wapambana na wafuasi wa Malema

Julius Malema
Polisi wa Afrika Kusini wametumia magrunedi ya kushtua watu wanaomuunga mkono kiongozi Vijana wa ANC mwenye ushawishi Julius Malema wakati kamati ya maadili ya chama hicho ikimuhoji.
Bw Malema mwenye umri wa miaka 30, anatuhumiwa kwa ‘kusababisha mgawanyiko’ katika chama na kuleta kukiletea sifa mbaya alipotaka serikali ya Botswana ipinduliwe.
Awali akiwa mshirika wa karibu wa Rais Jacob Zuma, Bw Malema amekuwa akimkosoa zaidi Rais huyo.
Watu wanaomuunga mkono waliwarushia mawe polisi ambao walikuwa wakiwazuia mjini Johannesburg.
Polisi wameweka vizuizi vya vyuma na nyaya kufunga mtaa unaoingia jengo la Luthuli House, yaliko makao makuu ya ANC mahali kikao hicho kinafanyika.
Mamia ya watu wanaomuunga mkono Bw Malema wako nje, wakiimba na kuchoma moto takataka.
Wengine walichoma moto fulana yenye picha ya Rais Zuma, huku wengine wakiimba ‘Zuma lazima aondoke.’
Bw Malema, ambaye ameshtakiwa kwenye Tume pamoja na viongozi wengine watano wa vijana anaweza kufukuzwa kwenye chama katika kikao siri kinachoendelea.
Aliwekwa kwenye majaribio na Kamati ya Maadili mwaka jana baada ya kukutwa na makosa ya kumkosoa Bw Zuma.
Bw Malema, akiwa bado anachunguzwa kwa kuhusu tuhuma za ufisadi na rushwa, amesema atakubali uamuzi wa kamati hiyo.
"Tunawajibika kwa matendo yetu na tuko tayari kwa chochote. Tumekuwa tukisema siku zote kuwa ANC ndiyo hatima yetu, ikiwa hatima yetu itaondolewa basin a iwe hivyo," alisema.

Julius Malema ni nani?

Julius Malema, kiongozi wa Vijana wa ANC
  • Alizaliwa 1981, alijiunga na ANC akiwa na miaka 9
  • Alipata mafunzo ya kijeshi miaka ya 1990
  • 2008:alichaguliwa kiongozi wa Vijana wa ANC
  • 2008: aliapa ‘kuua’ kwa ajili ya Jacob Zuma
  • 2009: asema mwanamke ambaye Zuma alituhumiwa kumbaka ‘alifurahia kuwa naye’ –baadaye aliadhibiwa
  • Akatoa wito kwa migodi itaifishwe na mashamba yanayomilikiwa na wazungu yachukuliwe.
  • 2010: alizdhibiwa kwa kumdharau Zuma
  • 2011: alihukumiwa kwa kuimba "Ua kaburu [Wakulima wa kizungu]"
  • Alitoa wito serikali ya Botswana ipinduliwe
  • Alituhumiwa kwa kuishi maisha kifahari

Kauli za utata

Mwandishi wa BBC anasema kiongozi huyo wa Vijana ametoa wito sekta ya madini itaifishwe na kwamba umiliki wa mashamba ya wazungu una ubia na viongozi wa chama hali ambayo imempa umaarufu zaidi wa kisiasa katika jamii ya weusi wanaokabiliwa na ufukara.
Mwandishi wa BBC Karen Allen amemwelezea Bw Malema kuwa ni ‘mwenye ushawishi mkubwa kwa viongozi na mwanasiasa’ ambaye kundi lake la vijana linailetea ANC kura 350,000 na ushawishi kwa viongozi waandamizi wa anc wanaotaka kupandishwa vyeo.
Hatua za kinidhamu dhidi yake zitaleta picha ya mbio za uchaguzi wa chama hicho mwakani.
Nia ya Bw Zuma kutaka kipidni cha pili cha Urais wa ANC itakuwa na nguvu iwapo umaarufu wa Bw Malema utatupiliwa mbali, mwandishi wa BBC anasema.
Iwapo, itakavyokuwa, kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa atatoka kwenye kikao hicho akiwa na uanachama wake, Rais Zuma atakabiliwa na hatima isiyotabirika, anasema.
Kwa muda mrefu kiongozi huyo wa vijana amekuwa mwenye utata.
Alikuwa mtu muhimu aliyemsaidia Bw Zuma kuchukua udhibiti wa ANC kutoka kwa mtangulizi wake Thabo Mbeki mwaka 2008 akampigia kampeni kali katika uchaguzi wa 2009 ambao ulimweka madarakani Bw Zuma.
Lakini Jumatatu, alisema hakuwa na uhusiano wowote binafsi na Rais isipokuwa wa kikazi.
Mwezi Mei 2010, alilazimishwa kuomba radhi hadharani kufuatia safari yake Zimbabwe iliyokuwa na utata ambako alitangaza kwamba ANC inamuunga mkono Rais Robert Mugabe wakati Bw Zuma alikuwa mpatanishi wa mgogoro wa serikali ya muungano nchini Zimbabwe.
Bw Malema aliadhibiwa na ANC kwa kumfukuza mwandishi wa BBC kwenye mkutano waandishi wa habari na kutotii amri za chama kwa kukataa kuacha kuimba wimbo maarufu uliokuwa na ushawishi wakati wa ubaguzi wa rangi ‘Ua kaburu[mkulima mzungu]

No comments:

Post a Comment