Makao makuu ya Tanesco Ubungo
PATO la Taifa limeendelea kushuka kwa asilimia 0.5 huku sekta za madini, elimu, afya, viwanda, uvuvi na nishati zikiathirika kwa kiasi kikubwa chanzo kikuu kikiwa ni upungufu wa umeme nchini.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, kutoka Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya takwimu za robo mwaka unaoanzia Aprili hadi Juni.
Oyuke alisema kwa mujibu wa takwimu hizo, Pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo pato hilo lilikuwa kwa asilimia 7.2, hivyo katika robo mwaka ya Aprili-Juni, pato hilo limeshuka kwa asilimia 0.5.
“Ukuaji wa Pato hilo kwa robo mwaka 2011 Januari hadi Machi ulikuwa ni asilimia 5.8 ambalo bado liko kwenye hali ya chanya, tunategemea katika vipindi viwili vya robo mwaka vilivyobakia hali itakuwa nzuri zaidi,” alisema Oyuke.
Alisema kutokana na hali hiyo, sekta kadhaa zimeonekana kuathirika kutokana na kushuka kwa uzalishaji ambapo kwa sekta ya uvuvi, ukuaji wake ni asilimia 0.7 ikilinganishwa na asilimia 1.9 mwaka jana, kushuka huko kunatokana na ongezeko dogo la mahitaji ya samaki katika soko la ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wa uchimbaji madini na mawe, katika robo mwaka ya Aprili-Juni imekuwa kwa asilimia 5.8 ikilinganishwa na asilimia 20.5 ya mwaka jana, uzalishaji viwandani ulishuka kwa asilimia 6.2 robo mwaka ya mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 7.5 mwaka jana.
“Kushuka kwa kasi ya ukuaji katika sekta hiyo ya uzalishaji kwa asilimia 1.3 kulitokana na kutopatikana kwa umeme wa uhakika kulikoathiri shughuli za viwanda nchini,” alisema mtaalamu huyo.
Alisema katika sekta ya nishati na umeme uzalishaji ulishuka na kufikia asilimia 3.1 mwaka huu kutoka asilimia 10 mwaka jana, shughuli za biashara rejareja, ukarabati wa magari na pikipiki zilishuka kasi kwa asilimia 6.0 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 9.6 mwaka jana. Hali hiyo, ilichangiwa na kupungua kwa bidhaa zilizotengenezwa nchini.
Aidha, alisema upangishaji nyumba na shughuli nyingine za biashara zilikua kwa asilimia 6.3 ikilinganishwa na asilimia 5.6 mwaka jana, kilimo kilikua kwa asilimia tatu robo mwaka ya pili mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 2.9 mwaka jana.
Shughuli za uendeshaji Serikali nazo zilishuka kwa asilimia 5.8 robo ya pili ya mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka jana, utoaji elimu ulishuka kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 7.1 mwaka jana na huduma za afya zilishuka na kufikia asilimia 4.0 ikilinganishwa na asilimia 6.3 mwaka jana.
Naye Mhadhiri wa Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hajji Semboja alisema pamoja na kwamba kushuka huko kwa Pato la Taifa kuko katika hali ya chanya, bado watunga sera wanahitajika kutumia takwimu hizo vizuri na kusawazisha yote yaliyosababisha kushuka huko kwa Pato la Taifa.

No comments:
Post a Comment