PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Sunday, 11 September 2011

KWA MWENDO HUU, YANGA KAZI IPO


Kikosi cha yanga
Ni kauli ambayo ilikuwa ikizungumzwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kumalizika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Ruvu Shooting Stars Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ni kauli nzito, lakini pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo huo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting Stars uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga ambayo ni bingwa mtetezi sasa imefikisha pointi tatu kwa michezo minne iliyocheza ikishika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14, matokeo ambayo yanawanyima raha mashabiki wake.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kushambuliana kwa zamu, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili baada ya kila timu kukosa mabao mengi ya wazi.

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Jerry Tegete, Julius Mrope na Rashid Gumbo walipata nafasi nyingi za kufunga, lakini umaliziaji ulikuwa tatizo.

Ruvu Shooting ilikuwa ya kwanza kufunga, baada ya mshambuliaji Abdallah Juma kufanya kazi nzuri na kumtengenezea pasi Paul Ndauka aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao kwa shuti lililomshinda kipa Yaw Berko.

Dakika 15 za mwisho, lango la Ruvu Shooting lilikuwa katika hekaheka, ambapo Kenneth Asamoah aliyetokea benchi alisawazisha kwa shuti baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Kigi Makasi na Davies Mwape.

Katika mchezo huo, Yanga ilimpoteza kiungo wake mshambuliaji, Haruna Niyonzima baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Awali alioneshwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya, kisha akaoneshwa kadi nyingine ya njano iliyoambatana na nyekundu baada ya kujiangusha makusudi eneo la penalti.

Mashabiki na baadhi ya wachezaji wa Yanga mara kadhaa walikuwa wakimlalamikia Mwamuzi Alex Mahagi kutoka jijini Mwanza, kwa madai baadhi ya maamuzi yake hayakuwa sahihi na haikuwa ajabu baada ya mchezo mashabiki kuanza kurusha chupa za maji uwanjani.

Kocha wa Yanga, Sam Timbe alisema kwamba wachezaji wake wamejaribu kucheza, lakini hawakuwa na matokeo mazuri.

Wakati huohuo, Simba na Azam leo zinachuana kwenye uwanja huo katika mfululizo wa ligi hiyo, ambapo Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa, huku Azam ikiwa nafasi ya nane ikiwa na pointi nne.

No comments:

Post a Comment