Arsenal yadorora yalazwa 4-3 na Rovers
Blackburn imeweza kupata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya England msimu huu na kumpunguzia ugonjwa wa moyo meneja wao Steve Kean baada ya kuwa nyuma lakini wakafanikiwa kuilaza Arsenal mabao 4-3 katika uwabnja wa Ewood Park.
Gunners walikuwa ndio wa kwanza kupata bao lililofungwa na Gervinho kutoka umbali wa yadi 12 lakini Blackburn walisawazisha kwa bao rahisi lililowekwa wavuni na Yakubu.
Mikel Arteta akaifungia Arsenal bao la pili kwa mkwaju safi wa yadi 18 kabla Alex Song hajajifunga mwenyewe.
Yakubu tena akaipatia Blacburn bao la tatu na kufanya ubao wa matokeo usomeke 3-2, na muda mfupi baadae Laurent Koscielny akajifunga mwenyewe kabla ya dakika za mwisho Marouane Chamakh kuipatia Arsenal bao la kufutia machozi.
Kabla ya mechi hiyo mashabiki wa Blackburn walifanya maandamano wakitaka meneja wao Kean atimuliwe.
Wiki nzima meneja huyo alikuwa akijigamba kwamba yeye ni meneja anayefaa kwa klabu hiyo ya Blackburn na matokeo ya mechi hiyo dhidi ya Arsenal yanaweza kumfariji na kumuweka mahali pazuri kulinda nafasi yake.
No comments:
Post a Comment