Wednesday, 5 October 2011

Kenya
Uganda kupambana na Kenya
Taifa
Taifa Stars

Moto utawaka Jumamosi hii mjini Kampala katika uwanja na Namboole wakati mahasimu wa jadi Uganda Cranes itamenyana na Harambee Stars ya Kenya.
Mechi hiyo muhimu huenda ikaamua ni timu ipi katika kundi J itafuzu kwa fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Angola nayo pia inawania nafasi hiyo na endapo itashinda Guinea Bissau na Kenya ichape Uganda basi Angola ndio itakayofuzu.

Mashabiki

Maelfu na maelfu ya mashabiki wanatarajiwa kushuhudia mechi hiyo ambayo ndiyo inayozungumziwa zaidi Afrika Mashariki na Kati. Tangu mwaka wa 2008 Sudan iliposhiriki fainali ya mashindano haya hamna timu nyingine ya eneo hili imefuzu. Mwaka wa 2006 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo ilikuwa timu pekee ya Afrika Mashariki na Kati nchini Misri, na mwaka jana hakuna timu ya eneo hili ilikwenda Angola kwa mashindano hayo.
Uganda ina hamu sana ya kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1978 ambapo walifuzu kwa mechi ya fainali wakanyamazishwa na Ghana. Ndio kwa maana itajumuisha wachezaji wake wote wa kulipwa kuona kwamba vijana wa nyama choma kutoka Kenya wanarudi nyumbani mikono mitupu.

Lazima washinde

Miongoni mwa wachezaji wa kulipwa Uganda Cranes inategemea sana kwa ushindi ni David Obua na makipa Abbey Dhaira na Brian Umony.
Kocha Bobby Williamson wa Cranes ana uhakika watashinda mechi hiyo lakini anakubali wana kibarua kigumu hasa kwa sababu kiungo matata wa Harambee Stars McDonald Mariga atakuwa uwanjani pamoja na mfungaji matata Dennis Oliech.
Kwa ujumla Uganda Cranes na Sudan ndizo timu za Afrika Mashariki na Kati ambazo zina matumaini makubwa ya kufuzu lakini lazima washinde mechi zao.

Mechi ngumu

Sudan inakutana na Ghana mjini Khartoum timu zote zikiwa na pointi 13 lakini Ghana iko juu kwa sababu ya wingi wa mabao. Mfungaji hodari wa Ghana Asamoah Gyan ambaye sasa anachezea Al-Ain ya Imarati kwa mkopo kutoka Sunderland anasema mechi ni ngumu lakini watashinda. Gyan yuko na wenzake Nairobi wakijiandaa kwa mechi hiyo.
Katika kundi H Burundi ni ya pili na pointi tano hivyo basi wana nafasi nzuri ya kuwa miongoni mwa timu bora zitakazofuzu kama watashinda Ivory Coast kwenye mechi ngumu ugenini.
Rwanda ni ya mwisho kundi hilo na ziara yao ya Benin ni ya kitalii.
Tanzania ni tatu kundi D na pointi tano, Morocco ikiwa mbele na pointi nane na ya pili ni Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tanzania itakuwa ugenini na Morocco. Kama Harambee Stars ya Kenya, Tanzania pia inategemea miujiza ifanyike ili wafuzu lakini matumaini yao ni haba.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nayo pia ina matumaini kam,a itashinda Cameroon nyumbani na kupata nafasi ya timu mbili bora zitakazochukua nafasi ya pili kati ya kundi A hadi J. DRC ni ya tatu kundi E na pointi saba. Senegal, ambayo tayari imefuzu, ni ya kwanza na pointi 13 huku Cameroon ikiwa ya pili na pointi nane..
Timu ambazo zimefuzu tayari ni Equatorial Guinea, Gabon (wote wenyeji),Botswana, Ivory Coast, Senegal na Burkina Faso. Jumla ya timu kutoka mataifa 16 zitashiriki fainali hizo

No comments:

Post a Comment