Thursday, 22 September 2011


Hatuhitaji ushahidi,kumtimua Chenge!

Siku chache baada ya serikali kumpaka sabuni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) kuwa hahusiki kwa namna yoyote na kashfa ya ununuzi wa rada, Chama Cha Mapinduzi kimesema hakihitaji ushahidi wa Mahakama kumchukulia hatua kada huyo. 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema kauli ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, haiwezi kuathiri uamuzi wa chama hicho wa kumtaka Chenge ajivue nyadhifa alizonazo ndani ya chama hicho na asipofanya hivyo, atavuliwa kwa nguvu. 

Akizungumza jana, Nape alisema chama ni chombo cha juu kuliko Serikali, hivyo uamuzi uliofanywa kwenye kikao halali, utaendelea kusimama hata kama Serikali itaendelea kumsafisha Chenge. Uamuzi wa kumchukulia hatua Chenge ulichukuliwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa. 

“Uamuzi ulichukuliwa na kikao halali cha chama kuwawajibisha watuhumiwa wa masuala ya ufisadi, wakiwamo watuhumiwa wa rada,” alisema Nape. 

Politician huyo kijana aliongeza kuwa hakuhitajiki ushahidi wa mahakamani kumchukulia hatua Chenge, bali kinachohitajika ni mtazamo wa jamii dhidi ya mtuhumiwa. “Yawezekana wenyewe Serikali hawana ushahidi wa kuwapeleka mahakamani, lakini sisi chama hatuhitaji huo ushahidi wa kumchukulia Chenge 

No comments:

Post a Comment