Thursday, 22 September 2011


Ghasia Zambia baada ya uchaguzi

Ramani ya Zambia
Ramani ya Zambia
Ghasia zimezuka katika miji miwili ya kaskazini mwa Zambia ambako wafuasi wa upinzani wanalalamikia kucheleweshwa matokeo ya uchaguzi wa Jumanne.
Mkuu wa Polisi wa jimbo hilo maafuru kwa uzalishaji Shaba ameliambia shirika la habari la Reuters watu wamejitokeza katika barabara za mji wa Kitwe na Ndola wakivurumisha mawe.
Mwandishi wa BBC anasema ghadhabu hizi zimechochewa na agizo la serikali kupiga marufuku vyombo vya habari kutangaza matokeo bila ya idhini ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Rais Rupiah Banda anakabiliwa na changamoto kali kutoka mpinzani wake wa karibu Michael Sata.
Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda akiwa Lusaka kilomita 300 kusini mwa Kitwe, anasema taarifa kuhusu ghasia tayari zimeshafika katika mji mkuu na kuwa watu wanaogopa sasa kwenda mjini kwa hofu ya kuzuka ghasia.
Tunajaribu kukabiliana na hali hii, kuna ghasia Kitwe na Ndola
Mkuu wa Polisi wa Mkoa Martin Malama akiongea na shirika la habari la AFP.
Huko Kitwe, waandamanaji waliteketeza soko moja usiku na Polisi wameweka vizuwizi katika mji wa Wusaikile.
Matokeo ya hivi punde yanaonesha Bw. Sata anaongoza kwa 47% ya kura katika maeneo 33 ya uwakilishi kati ya 150 ya nchi nzima.
Rais Banda alimshinda Bw Sata kwa kura 35,000 katika uchaguzi wa mwaka 2008, matokeo yaliozusha ghasia kutoka upande wa upinzani katika ngome zao za mijini.
Tangu uchaguzi wa mwaka 2008, watu wengine milioni moja wamejiandikisha kuwa wapiga kura,wengi wao vijana wasio na ajira.
Mwandishi wetu anasema matokao kamili yanatarajiwa kutangwa leo jioni.

No comments:

Post a Comment