Waasi wasonga mbele kuidhibiti Tripoli
Tripoli imeshuhudia mwendelezo wa mapigano na vikosi vinavyomtii Gaddafi katika mji wa Tripoli siku moja baada ya waasi kuteka makazi ya Gaddafi.
Kumekuwa pia na makombora mapya ya NATO.
Waasi walipigana na wanaomuunga mkono Gaddafi katika maeneo kadhaa ya kusini na katikati ya mji, kikiwemo kikosi kingine kutoka mashariki mwa uwanja wa ndege.
Mlipuko wa mabomu mawili ulitikisa mji wakati ndege za NATO zilipopita angani.
Haijulikani Kanali Muammar Gaddafi aliko lakini alitoa ujumbe wa kutokujisalimisha jana usiku.
Katika ujumbe wake, amesema alifanya ‘mbinu’ kurudi nyuma kuondoka kwenye makazi yake ya Bab al-Aziziyalakini mwanadishi wa BBC BBC Wyre Davies anaripoti kutoka mjini humo kuwa hakuna anayeamini ripoi ya matukio hayo.
Wadunguaji wanaomuunga mkono Gaddafi walionekana ndani ya Bab al-Aziziya yenyewe baada ya kuvamiwa na waadi na vita ya kuidhibiti kikamilifu Tripoli inaendelea.
Kanali Gaddafi inadhaniwa kuwa ana wafuasi wengi katika miji mikubwa miwili ya Sirte ulio pwani na Sebha kilometa 650 (400 maili ) kusini mwa mji, ambako mapigano yalizuka wiki hii.
Wakati huo huo, Baraza la waasi la Mpito (NTC) likimaanisha kuanza kazi ya kuijenga upya Libya iliyosambaratishwa na vita, linafanya kikao na wafadhili nchini Qatar huku ujumbe wa maafisa ukihama kutoka ngome ya waasi ya Benghazi kwenda Tripoli.
'Gaddafi atoweka'
Milio ilisikika tena Jumatano asubuhi karibu na hoteli ya Rixos mjini Tripoli ambako wageni wa kimataifa 35, wengi wao wakiwa waandishi wa habari wamezuiliwa na wanaomuunga mkono Gaddafi.
Mwandishi wa Reuters ambaye alikuwa katika eneo hilo muda wa mchana (10:00 GMT) alisikia milio ya risasi na silaha nyingine nzito zikitumiwa na pande zote mbili dhidi ya maeeneo muhimu.
Kiongozi mmoja wa waasi ameliambia shirka la habari la AFP kuwa vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi vilikuwa vimejificha katika barabara kuelekea uwanja wa ndege.
Wakazi wa Tripoli wenye silaha walisalia kuwa makini na kuendelea na zamu za kulinda vizuizi kwa msaada wa waasi, anaripoti mwandishi wa BBC Rana Jawad kutoka mjini humo.
Haikuwa wazi NATO walikuwa wanalenga wapi lakini taarifa ambayo haijathibitishwa kutoka televisheni ya Al-Arabiya ilisema silaha za upande wa serikali zimekuwa zikishambulia miji ya Zuara na Ajelat, magharibi wa mji mkuu.
Haijulikani iwapo Kanali Gaddafi na familia yake walikuwa Bab al-Aziziya siku ya Jumanne wakati yaliposhmbuliwa lakini kiongozi huyo akaahidi kifo au ushindi katika hotuba yake.
Katika taarifa yake iliyotangazwa na televisheni inayomuunga mkono Jumanne usiku kiongozi huyo alisema "Nilitoka kwa siri nyumbani kwangu Tripoli bila watu kunitambua na niliwakuta vijana mitaani. Kwa kweli , sikuhisi kama Tripoli inaanguka au kwamba kuna watu wameingia."
Familia ya Gaddafi inaaminika imekuwa na upenyo katika nyumba nyingi kwa ajili ya usalama mjini Tripoli na nje, na haijafahamika wazi iwapo makazi ya Kanali katika mji wa Sirte, ambayo imekuwa ngome ya wafuasi wake.
Sebha ina kambi muhimu ya jeshi na kikosi cha anga, iwapo Kanali Gaddafi anaweza kufika huko, itampa fursa rahisiya kutorokea njia ya jangwani kuingia nchi za Niger na Chad, kwa mujibu wa shirika la Habari la AP.
Msemaji wa waasi ameiambia BBC majadiliano yalikuwa yanaendelea na watu Sebha na Sirte kwa ajili ya kumaliza kwa mgogoro huo kwa amani.
Ombi la Ufadhili zaidi
Wawakilishi wamekuwa wakijiandaa kwa mazungumzo ya hali ya juu nchini Qatar na ujumbe mwingine Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uturuki na Falme za Kiarabu kujadili namna ya kuendeleza Libya baada ya Gaddafi.
Kiongozi wa Baraza la muda la Kitaifa la NTC Mahmoud Jibril, alisema wanatafuta $2.5 bilioni (£1.5 bilioni) kama msaada wa dharura.
Kipaumbele cha haraka ni kuwalipa mishahara wafanyakazi na kugharamia misaada ya kibinadamu lakini kwa mipangoya muda mrefu pesa zitahitajika kukarabati miundombinu ya mafuta nchini humo.
Bw Jibril anakadiria kuwa Libya ina amana iliyositishwa ya thamani ya $160-170 bilioni mali isiyohamishika. Marekani imesema itajaribu kuachilia kiasi cha mpaka $1.5bilioni ya mali za Libya.
Waasi walivamia Tripoli mwishoni mwa wiki na Jumanne walivunja ngome ya makazi ya Kanali Gaddafi.
Machafuko ya kisiasa ya kuupinga utawala wa miaka 41 wa Kanali Gaddafi yalianza Februari. Waasi walichukua eneo la Mashariki na baadhi ya maeneo ya magaharibi kabla ya kuelekea katika mji mkuu mwishoni mwa wiki.
Mashambulizi ya anga ya NATO yamekuwa yakilenga vikosi vya Gaddafi, yakitimiza jukumu la UN la kuwalinda raia. Wakosoaji wanashutumu muungano huo kushirikiana na waasi.
No comments:
Post a Comment