Sunday, 21 August 2011

MTOTO MVIVU AMWITIA MAMA YAKE POLISI



Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka kumi na moja nchini Ujerumani, amepiga simu polisi kumshtaki mama yake kwa kumfanyisha kazi za nyumbani.
Mama
Mama aitiwa polisi
"Hello, mama yangu ananifanyia kazi za nyumbani kwa nguvu" amesema kijana huyo alipopiga simu polisi.
Mtandao wa news.com umesema kijana huyo aitwaye Leon yuko katika likizo yake baada ya shule kufungwa.
Polisi wamemuuliza ni kazi gani hasa analazimishwa kufanya? "Natakiwa kusafisha kibaraza cha nyumba, nafanya kazi siku nzima" amelalamika kijana huyo.
Mama wa kijana huyo, amewaambia polisi kuwa mtoto wake amekuwa akitishia kumshtaki kwa polisi kwa wiki kadhaa sasa.
"Sasa hivi ameambiwa aokote makaratasi kidogo, ndio akaamua kupiga simu polisi" amesema mama huyo. "yaani yeye hucheza siku nzima, ukimwabia asafishe chumba chake tu, anaanza kusema analazimishwa kazi" amesema mama huyo.
Polisi katika mji wa Aachen lilipotokea sakata hilo wamefunga kesi hiyo

No comments:

Post a Comment