Sunday, 7 August 2011

MR 0% FACE TO FACE WITH MR 100%

Afadhali leo nimekuona nilikua nakutafuta saana mambo vipi? shega kwa saana mwana nambie...nilikua nakutafuta ili nikujulishe kwamba nimebadilisha jina, haa yaani huitwi tena Omari Omari...ndio baada ya kumaliza university nimeamua nijiite Mr 100%..du poa saana jina sio baya......hata mimi pia nimebadili jina baada kuamua mwenyewe kwamba sitosoma hata wazazi wangu wamelikubari naitwa Mr 0%...ahahaha aibu aibu tehe tehe..kwahiyo hapa naongea na jongoo, kinyonga, na mtu chizi tena wajalalani, Mr 0% kahamaki na kusema tafadhari naomba tuheshimiane na kabla sijakukata hio shingo yako naomba unambie nini maana ya hayo majina?... (1) nimekuita jongoo kwakua hana tofauti na wewe kwani alipoambiwa achague kati ya miguu na macho kwa ujinga wake amechagua miguu, ndio maana hadi leo hii hajui aendako huku akiandamwa na mitusi ya nguoni toka kwa binaadamu wakimuona utasikia hilo jongoo lipekueni na likome kutufuata fuata na kiji litupieni hukohuko lisiludi tena,..(2) na kinyonga pia alipo ulizwa kati ya mwendo kasi na mdogo mdogo akachagua mdogo mdogo, matokeo yake kwenye kasheshe ye ndio wakwanza kufa, (3) na mtu chizi tena wa jalalani, kunatajili mmoja ameenda kijijini amerudi na mkulima mjini akamwekea kati ya $ bilion kumi na shilingi bilion 5..yeye amechagua shilingi bilion 5..watu walipo mcheka akauliza mnacheka nini?...alipo fafanuliwa na kwavile watu walimcheka ndio hivyo tena mtu wa watu kawa chizi hadi hii leo, sasa hizi ndio faida za kusoma hadi university la sivyo nisingejua hivi vitu upo hapo? anaulizwa Mr 0% ana mjibu nipo tena gado asante saana kwa ufafanuzi wako,yaani watu wanakua wendawazimu kwa kuchekwa tena kwa makosa yao mimi sitaki yanikute hayo naludia tena asante ndugu yangu watu kama nyinyi wachache saana kwenye hii dunia, mimi nitajiita 100% kama wewe endapo utanijibu hili swali langu?...wewe unaswaligani la mimi kushindwa kujibu wewe uliza tu, KUNA AJALI MBAYA SAANA IMETOKEA MPAKANI MWA, INDIA NA PAKISTANI YA MABASI MAWILI USO KWA USO HIVI (MAJELUHI) WATAZIKWA WAPI?..Mr 100% anamjibu Mr 0% ya kwamba wa pakistani watazikwa pakistani na wale wa india watazikwa india, mwendo wenyewe kama ndio huu hakiyamungu wamajalalani tutakua wengi mmmno mimi nilijua labda utasema, majeluhi hawazikwi bali wanakimbizwa mahospitalini,..angalizo wadau hii kesi inaunguluma mahakamani,..lakini mpembuzi wenu papaya au mjini shule..anaifuatilia kwa karibu wala msikonde.

No comments:

Post a Comment