PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Monday, 3 October 2011

PICHA YA LEO


Mbunge mteule wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu akipongezwa na mke wake, Maria Magdalena Kafumu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi Mdogo uliofanyika Oktoba 2. Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (nyuma ya Kafumu) na kulia kwa Mukama ni Katibu wa NEC wa Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma. (Na Mpigapicha Maalumu)

Arsenal yafungwa licha ya kung'ara

Wachezaji wa Arsenal
Wengi wanaamini Arsenal ilicheza vyema Jumapili licha ya kufungwa na Tottenham
Bao la Kyle Walker kutoka yadi 25 liliiwezesha Tottenham kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani White Hart Lane, dhidi ya wageni Arsenal, katika mechi ya kusisimua sana kaskazini mwa mji wa London.
Mlinzi Walker aliweza kufunga bao hilo katika dakika ya 73.
Bao la kwanza la mechi hiyo la Tottenham lilifungwa na Rafael van der Vaart katika kipindi cha kwanza, baada ya kuupokea mpira kutoka kwa Emmanuel Adebayor.
Aaron Ramsey aliweza kusawazisha katika kipindi cha pili, baada ya kupata mpira kutoka kwa Alex Song.
Ingawa Wojciech Szczesny angeliweza kuokoa mkwaju wa Walker, ni lazima ikumbukwe kwamba aliweza kuzima mikwaju ya Adebayor na Jermain Defoe.
Gareth Bale bale alikuwa pia na nafasi ya kuiwezesha Spurs kufunga mkwaju wa tatu, lakini juhudi zake ziliangukia patupu.
Katika mechi nyingine zilizochezwa awali Jumapili, Bolton ikichezea nyumbani uwanja wa Reebok ilifungwa na wageni Chelsea magoli 5-1.
Swansea nayo inaweza kujivunia ushindi baada ya kuwakaribisha Stoke na kuwafunga magoli 2-0.
Lakini hakuna timu ambayo imethibitisha ugumu wa ligi kuu ya Premier kama QPR, kwani walipoitembelea Fulham, walizabwa magoli 6-0, na kuondoka pasipo hata kupata moja la kufutia machozi.

Upigaji kura umemalizika Igunga

Wananchi wa Tanzania katika jimbo la Igunga, katikati mwa nchi, wamemaliza kupiga kura.
Bendera ya Tanzania

Inakisiwa kuwa nusu wa wapigaji kura wamejitokeza, karibu sawa na wakati wa uchaguzi mkuu.
Kiti hicho kilichoachwa wazi na Mbunge Rostam Aziz wa chama tawala cha CCM, kimeona mashindano hasa kati ya vyama vitatu vikubwa - CCM, CHADEMA na CUF.
Wakuu wa uchaguzi wanakisia kuwa matokeo huenda yakawa tayari leo, Jumapili usiku

19 wauawa katika kijiji Nigeria

Waathirika wa mashambulio kaskazini mwa Nigeria

Takriban watu 19 wamepigwa risasi au kukatwa kwa mapanga katika tukio baya zaidi kwenye kijiji kimoja kilichoko kaskazini magharibi mwa Nigeria, polisi wamesema.
Walioushuhudia wanasema watu karibu 150 walivamia kijiji cha Lingyado, katika jimbo la Zamfara karibu na mpaka wa Nigeria na Niger, wakiwa na bunduki na mapanga.
Msemaji wa polisi anasema inaonekana kama ni uvamizi wa kulipiza kisasi kufuatia uvamizi kama huo mwezi wa nane.
Maafisa wa usalama wako katika eneo hilo kujaribu kutuliza hali.
Msemaji wa polisi Sunusi Amiru anasema watu wengine sita walijeruhiwa katika uvamizi huo na kwa sasa wanatibiwa.
" Tuko imara kabisa, na tunawasaka washukiwa, tumepeleka maafisa zaidi kwenye maeneo yaliyo hatari zaidi," aliambia shirika la habari la Reuters.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria Jonah Fisher anasema walioathirika walivamiwa wakati wakitoka nje ya nyumba zao

ICC yataka uchunguzi Ivory Coast

Moreno Ocampo
Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imempa idhini mkuu wake wa mashtaka kuanza uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa Ivory Coast.
Watu wapatao 3,000 waliuawa na wengine 500,000 kuachwa bila makao katika ghasia hizo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Alassane Ouattara alichukuwa hatamu za uwongozi mwezi Aprili baada ya miezi minne ya mvutano na mwenzake Laurent Gbagbo aliyekataa kukubali ushindi wa Ouattara.
Vikosi tiifu kwa mabwana hawa wawili vyote vimeshutumiwa kwa uhalifu na ukiukaji haki za binadamu.
Majaji wa ICC pia walimtaka mkuu huyo wa mashtaka Luis Moreno-Ocampo, atoe majibu ya uchunguzi wake katika kipindi cha mwezi mmoja kuhusu taarifa zaidi za uhalifu zilizotekelezwa kati ya mwaka 2002 na 2010.
Uchaguzi wa mwezi November ulinuiwa kuwaleta pamoja wananchi na kuiunganisha nchi hiyo iliyogawanywa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002.
Ivory Coast - mzalishaji mkubwa wa zao la Kakao duniani- ilionekana wakati mmoja kuwa eneo la amani na ufanisi la Afrika Magharibi .
Nchi hiyo wakati huu inaonekana kukabiliana na mgawanyiko na pasuko unaozingatia ukabila, dini na uchumi.
Bw Gbagbo wakati huu anahudumia kifungo cha nyumbani na ameshtakiwa na uporaji maji , wizi wa kutumia nguvu na ufujaji mali.
Alikataa kata kata kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Rais, licha ya Umoja wa Mataifa kumtangaza Bw Ouattara adui wake wa jadi kuwa mshindi.

Sunday, 2 October 2011


Waandamanaji wazinga Wall Street

Polisi mjini New York wamewakamata watu zaidi ya 700 ambao walizinga daraja moja ya mji huo iitwayo Brooklyn Bridge, walipoandamana kupinga kile wanachokiona kama uroho wa wafanya biashara ya fedha.
Waandamanaji wa New York
Afisa wa serikali alisema walikamatwa kwa sababu walizinga magari kupita.
Waandanamanaji hao, kwa majuma mawili, walikuwa karibu na barabara ya masoko ya fedha, Wall Street.
Wanaharakati hao wanaojiita "Anti-Wall street", yaani "wapinzani wa Wall Sreet", kwanza walikuwa kwenye bustani ndogo mjini humo kwa wiki mbili, kupinga fedha zilizotumika kusaidia mabenki mwaka 2008, na ushawishi mkubwa wa makampuni kwenye siasa za nchi.
Kikundi cha internet, kiitwacho Adbusters, ndicho kilichopanga mkusanyiko huo.
Kikundi kiitwacho "Occupy Wall Street" kina wafuasi tofauti, wanasema wamevutiwa na harakati za jamii za Uspania na vuguvugu la nchi za Kiarabu.
Wana biramu zinazoonesha malengo yao - kama kuwalenga wanaopendelewa na mfumo wa kodi, uroho wa makampuni na wanataka amani.
Piya wanapinga utumizi wa nguvu na kile wanachoona kuwa ukosefu wa haki kwa wachache, wakiwemo Waislamu.
Wanaharakati hao piya wanapinga watu kunyang'anywa nyumba zao, kwa sababu wameshindwa kulipa deni la nyumba, ukosefu wa kazi, na serikali kuyasaidia mabenki mwaka wa 2008.
Watu wa filamu, kama Michael Moore na mchezaji sinema, Susan Sarandon, walipita kuwaunga mkono waandamanaji.
Kikundi hicho sasa kimeanza kupata wafuasi katika miji mengine mikubwa ya Marekani.

Mtalii wa Kenya amepelekwa Somalia

Serikali ya Kenya inasema mwanamke kutoka Ufaransa aliyetekwa nyara jana usiku, kutoka eneo la watalii Lamu amepelekwa Somalia.
Ngarawa katika pwani ya Lamu
Wamesema kuwa waliomshambulia walikimbia baada ya mapambano ya risasi, wakati walinzi wa mwambao na helikopta kuwaandama na kuwafikia wakiwa kwenye mashua ambamo wamembeba mtalii huyo.
Watekaji nyara kadha walijeruhiwa katika mapambano hayo.
Mwanamke huyo, akiwa na umri wa zaidi ya miaka 60 na mlemavu, alikuwa akikaa katika eneo la watalii karibu na Lamu.
Ufaransa sasa imewaonya watalii wasizuru eneo hilo.
Majuma matatu yaliyopita, kaskazini zaidi kwenye mwambao wa Kenya, mwanamke kutoka Uingereza alitekwa nyara na washambuliaji kutoka Somalia, ambao walimpiga risasi mumewe na kumuuwa

Kampeni za uchaguzi zaanza Tunisia

Kampeni zimeanza nchini Tunisia, za uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi -- ambao unafuatia mapinduzi ya mwezi Januari, yaliyomtoa Rais Zine El Abidine Ben Ali, ambaye aliondoka baada ya maandamno ya fujo.
Tunisia
Wapigaji kura watachagua wawakilishi wao katika bunge ambalo litakuwa na mwaka wa kutayarisha katiba mpya, kabla ya uchaguzi mwengine kufanywa.
Wawakilishi kama elfu-10 wa vyama 80 vya kisiasa wanashiriki katika uchaguzi huo.
Uchaguzi utafanywa tarehe 23 mwezi huu.