PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Saturday, 3 September 2011

HAYA NDIO MATOKEO YA MECHI ZA LEO


3/09/11  Libya  1-0 Mozambique
3/09/11-  Rwanda  0-5  Cote d’Ivoire
3/09/11-  Namibia 1-0  Gambia
3/09/11-  Cameroon  6-0 Mauritius
3/09/11- Tanzania 1-1   Algeria
3/09/11-  Malawi  0-0 Tunisie 
3/09/11-  Kenya   2-1 Guinea Bissau
2,/09/11  Ghana 2-0  Swaziland
3/09/11-19:00  Mali   Cap Vert
4/09/11- 15:00  Zimbabwe   Liberia
2,3,4/09/11  Guinea   Ethiopia
4/09/11   Madagascar Nigeria
4/09/11-15:00  Comoros   Zambia
2,3,4/09/11  Central Africa   Morocco
3/09/11-  Senegal   RD Congo
4/06/11- 16:30  Sierra Leone   Egypt

Ghana yailaza Swaziland 2-0

Ghana imeendelea kuongoza katika kundi lao la I kwa ajili ya mashindano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012, baada ya kuilaza Swaziland 2-0 mjini Accra siku ya Ijumaa.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana
Mshambuliaji wa Sunderland Asamoah Gyan aliifungia Ghana bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya nane.
Emmanuel Agyemang-Badu akaongeza bao la pili katika dakika ya 78 baada ya kuachia mkwaju wa umbali wa yadi 20.
Hata hivyo ushindi huo wa Ghana uliingia dosari kutokana na kuumia kwa mshambuliaji wao Gyan na alitolewa nje ya uwanja kabla ya mapumziko kutokana na kile kilichoonekana maumivu ya msuli wa paja.
Sasa kuna wasiwasi kama ataweza kucheza mechi ya siku ya Jumanne dhidi ya Brazil mjini London.
Black Stars ingeweza kushinda kwa mabao mengi lakini mkwaju wa nguvu wa Kwadwo Asamoah alioufyatua kiasi cha yadi 30 katika dakika za nyongeza ulipogonga mwamba na kutoka nje.
Matokeo hayo yana maana Black Stars inaongoza kungi lao kwa kukusanya pointi 13 huku wakibakiwa na mchezo mmoja tu.
Sudan wanaoshikilia nafasi ya pili, ambao wamezoa pointi 10, hawana budi kuwalaza Congo mjini Brazzaville siku ya Jumapili ili waweze kuwa karibu kabisa na Black Stars.

CHA CHANDU YA WEEKEND HII

Cha chandu kama hizi nitawapa kila weekend.

TANZANIA, ALGERIA NANI KUIBUKA MSHINDI LEO?




Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen (kushoto) akizungumza na wachezaji wake katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika jana jioni kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ya leo dhidi ya Algeria. (Picha kwa hisani ya Fullshangwe.)
Timu ya taifa, Taifa Stars leo inashuka dimbani kuikabili Algeria katika mechi ya kufa na kupona ya Kundi D la kuwania tiketi ya kufuzu fainali za mwakani za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2012).
Mechi hiyo itaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zote, Stars na Algeria iliyotua nchini juzi usiku, zina pointi nne na ili kufufua matumaini ya kushiriki AFCON 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Equatorial Guinea na Gabon, ni lazima zisake ushindi wa namna yoyote ile.

Akizungumza na gazeti hili jana, nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’, alisema kuwa wamejiandaa vyema na wanachoomba ni dua za Watanzania kukamilisha malengo yao ya kuibuka na ushindi wa nyumbani.

Nsajigwa alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao wamejipanga kupigana kufa na kupona na hiyo inatokana na kuimarisha kikosi chao pamoja na benchi la ufundi ikiwemo kuajiri kocha mpya Vahid Halilhodzic baada ya kumtimua wa awali, Rabah Saadane.

"Tunafahamu kwamba kesho (leo) tunakabiliwa na mtihani, tunaomba Mungu ili tushinde na kurejesha matumaini ya kufuzu fainali za Afrika," alisema nahodha huyo.

Alisema kwamba kila mchezaji amejipanga kucheza kwa juhudi na kwa kutumia faida ya uwanja wa nyumbani wanawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwahamasisha zaidi.

Katika kudhihirisha kwamba mechi hiyo ni ngumu kwa pande zote mbili, jana mchana makocha, Jan Poulsen wa Stars na Halilhozic wa Algeria walishindwa kutokea katika mkutano wa waandishi wa habari kama ilivyopangwa awali na kila mmoja kueleza kwamba amebanwa na programu za kiufundi na kwamba watakuwa tayari kuzungumza baada ya kumalizika kwa mechi yao ya leo.

"Makocha wamesema kwamba wamebanwa na programu zao na hii inaonyesha ni jinsi gani mechi ya kesho (leo) ni muhimu, wamesema watakuwa tayari kuzungumza baada ya mechi hapo kesho (leo)," alisema Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mkutano huo kati ya makocha na wanahabari ulipangwa kufanyika saa 6:00 mchana lakini utakangazwa kuahirishwa hadi saa 8:00 mchana, na muda mfupi baadaye, Wambura akaeleza kwamba makocha hao hawataweza tena kuzungumza na vyombo vya habari.

Ili kuhakikisha ushindi unapatikana Poulsen amewaita nyota wote saba wanaocheza nje ya nchi ambao ni Athumani Machuppa, Mbwana Samatta, Nizar Khalfan, Henry Joseph, Danny Mrwanda, Abdi Kassim 'Babi' na Idrissa Rajab wakati Halilhodic amewaita wachezaji wa nje 20 na wa ndani wanne. 

Mechi nyingine za Kundi D zinazotarajiwa kuchezwa leo ni Jamhuri ya Afrika ya Kati dhidi ya Morocco. Katika mechi nyingine za awali za kuwania kufuzu AFCON 2012, majirani Rwanda watawakaribisha Ivory Coast, Kenya watawavaa Guinea Bissau jijini Nairobi, Burundi watacheza nyumbani jijini Bujumbura dhidi ya Benin huku Uganda inayohitaji sare ili kufuzu watacheza ugenini dhidi ya Angola.