PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Saturday, 24 September 2011

NAIBU WAZIRI, AMPA MSHITUKO DR ASIE JUA ALIFANYALO

NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, ameelezea udhaifu wa utoaji huduma za afya kwa baadhi ya hospitali nchini, baada ya kwenda katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kuandikiwa dawa bila kujieleza kwa daktari.

Dk. Nkya alisema hayo wakati akizungumza na menejimenti, wafanyakazi na wanafunzi wa uuguzi na udaktari katika Hospitali Teule ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai, baada ya kupata hati rasmi ya kutambua kupanda hadhi kwa hospitali hiyo.

Huku akiitaja hospitali hiyo, Naibu Waziri alisema alifika hapo bila kujitambulisha huku amejifunika nguo hadi usoni akaingia kwa daktari ambaye hakumtaja jina, lakini daktari huyo alimwandikia dawa bila kumwuliza tatizo lake.

“Niliingia kwa daktari na kabla sijakaa, akaanza kuniandikia vipimo huku akinihoji kama nina homa na shinikizo la damu (BP), nilimjibu nitajuaje wewe ndiye mtaalamu, akanieleza tena natakiwa kupigwa picha za mionzi (X-ray), nilishangaa sana,” alisema.

Alisema kutokana na hali ile, alimweleza daktari husika kwamba anatakiwa amsikilize kabla ya vipimo, lakini katika hali ya kushangaza, alisisitiza kuwa anatakiwa kwenda kupigwa picha za X-ray.

“Niligundua kuwa daktari yule alikuwa amedhamiria na analosema nilijitambulisha kwamba mimi ni Dk. Lucy Nkya, Naibu Waziri … alipatwa mshtuko, nikamhoji kama ndivyo anavyotoa huduma kwa wananchi wa kawaida, nilimwonya nikaondoka,” alisema.

Alisema aliondoka na kuahidi kurejea wakati mwingine bila kutambulika, ili kuangalia mwenendo wa mtumishi huyo kama anatekeleza wajibu wake kulingana na sheria, kanuni na taratibu za utoaji tiba.

Akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo teule, alisema imekuwa miongoni mwa hospitali teule 34 nchini na kuwataka watumishi wake kuzingatia kanuni na taratibu za afya kwa kutoa huduma kulingana na viapo vya taaluma yao.

“Ninyi leo mmepata hati rasmi ya utambuzi kuwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Hai, hakikisheni mnatimiza wajibu wenu … hii sasa ni hospitali ambayo inatoa huduma kwa vigezo vya Serikali, nisingependa kusikia malalamiko dhidi yenu,” alionya.

Aliitaka Halmashauri ya Hai kutohamisha watumishi wa hospitali hiyo kwa namna yoyote na badala yake wajitahidi kukabili changamoto zilizopo ili iweze kutekeleza wajibu wake.

“Sasa Serikali itakuwa ikilipa mishahara na marupurupu kwa watumishi wa hospitali hii, tukisikia halmashauri mnahamisha watumishi au kutumia fedha zinazotumwa ili kufanyia vikao, safari za namna yoyote … tutawachukulia hatua kisheria,” alisema.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk . Saitore Laizer, aliiomba Serikali ianze kutoa ruzuku ya mishahara, dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa hospitali hiyo, ili wananchi wapate huduma kwa gharama nafuu kama ilivyo kwa hospitali zingine za umma.

Alisema changamoto nyingine ni uhaba wa watumishi unaosababishwa na kuhama kwa watumishi kutoka mashirika ya dini na ya binafsi kwenda serikalini, jambo ambalo limeiathiri hospitali hiyo hususani idara za meno na macho.

AHADI NI DENI, CHACHANDU YA WEEKEND HIYO

SWALI OF THE DAY, HUYU NI MWANAMKE AU DUME?

Wadau msikonde kama hamnajibu, nitakupeni
jibu hapo baadae.

Rais wa Zambia akubali kushindwa

Rais wa Zambia Rupiah Banda amekubali kushindwa kwake na kiongozi wa upinzani Michael Sata.
Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.
Rupiah Banda na Michael Sata
"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.
"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.
Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.
Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.
Mwandishi wa BBC Louise Redvers kwenye mji mkuu, Lusaka, alisema kuhusu tangazo hilo, wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.
Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.

Friday, 23 September 2011

BREAKING NEWZZZZZZ,MDADA WA KITANZANIA ASHINDA MILIONI £98 HUKO READING

Dada wenyewe ndio huyu

Sasa wadau msaada jamani? kwa yeyote anae mjua
huyu dada japo jina tupasiane maana nimehangaika
nimeshindwa zaidi ya kupata pic yake...ila inasemekana
kumetokea mtafaluku mkubwa huyu dada ana taka kuludi
africa serikali ya hapa haitaki eti wanasema kule ataenda
kufirisika. sasa kwanini hawataki?....vuteni subla wadau
nitafuatilia mpaka nijue nini kinachoendelea.




Aksante saana mdau reading kwa kunipa hii habari. 

SERENA NEEEEMA KEDEKEDE


Serena Williams ateuliwa kama balozi mwema wa UNICEF

Kusikiliza / Hamishia
serena williams (katikati)
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ( UNICEF ) leo limemteua bingwa wa mchezo wa tennis Bi Serena Williams kama balozi mwema wa kimataifa. Bi. Williams ni mmoja wa wachezaji wa tennis wenye mafanikio ya muda mrefu katika mchezo huu. Mchezaji huyo anayejulikana kwa uwezo wake kuwa mshindi katika mchezo huu, pia anajulikana kwa mchango wake nje ya mchezo.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la UNICEF Bw. Anthony Lake amesema kuwa Bi. Williams sio tu bingwa wa tennis lakini ni bingwa kwa watoto, hasa kwa utetezi wa elimu bora kwa watoto. Ameongeza kuwa anafuraha kubwa kwa Bi. Serena kujiunga kama balozi mwema wa Shirika la UNICEF na anatarajia kufanya kazi na Bi. Williams.
Kama balozi mwema wa UNICEF, Bi. Williams atatumia umaarufu na maslahi binfasi kusaidia utetezi wa haki ya elimu kwa watoto ambao ni ujumbe wa shirika hilo, kwa kupitia mpango wa shule Afrika and Asia.
Kwa habari zaidi tembelea: swahili radio ya umoja wa mataifa.

IMECHOMOKA PUNDE TU, HUKO KWA OBAMA


Ubaguzi wa rangi na kutovumiliana kunaendelea

Kusikiliza / Hamishia
watu waishi kwa maelewano
Miaka kumi iliyopita Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio la Durban na mpango wa kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambapo jumuiya ya Kimataifa ilitanabaisha kwamba hakuna nchi ambayo itasema iko huru bila ubaguzi na kutovumiliana. Leo ni miaka kumi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaadhimisha kwa kutathimini hatua zilizopigwa na nini kiendelee kufanyika.
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema suala hili bado ni tatizo ingawa hatua zimepigwa kukabiliana na matatizo ya ubaguzi, mauaji ya wageni na kutovumiliana. Amesema sheria zimeanza kushika mkondo, mipango ya kuchagiza utengamano na watu wamejiandaa vyema sasa kuchukua hatua na kulinda watu dhidi ya mauaji ya kimbari, ubaguzi wa rangi, mauaji ya kikabila na mifumo ya kisasa ya utumwa. Amesema ubaguzi dhidi ya Waafrika, watu wenye asili ya Afrika, Waasia, watu wa asili, wahamiaji, wakimbizi, makundi ya wachache, waromania na wengine lazima ukomeshwe

Ujumbe kwa wadau wote toka kwanza entertainment:
Tuupinge ubaguzi wa aina yoyote ile kwa nguvu zote
Aksanteni wenu papaya, mpenda amani... a k a ..Mzazi

KAZI NI KAZI WADAU, TUSICHAGUE