PATA HABARI MOTO MOTO, ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KUPITIA HAPA, TUPE MAWAZO YAKO TUYAFANYIE KAZI, TUPE HABARI ZOZOTE ULIZO NAZO TUTAZIWEKA HAPA,KWA MWENYE PARTY AINA YOYOTE INAYOHUSIANA NA MAMBO YA MUSIC, TAFADHARI ONGEA NA PAPAYA KUPITIA NAMBA HII..07501 202029..YUPO MACHO 24/7 BEI MAELEWANO.

Saturday, 27 August 2011


Askari mamluki Libya wanarudi kwao

Umoja wa Mataifa umeziomba pande zote katika vita vya Libya, kuzuwia vitendo vya kulipiza kisasi.
Wanajeshi wa Gaddafi
Taarifa hiyo imetolewa baada ya kuarifiwa kuwa wanajeshi wa Kanali Gaddafi wameuwa watu, na kwamba Waafrika waliokuwa wakipigana kwa niaba ya serikali piya wameshambuliwa.
Huku kukiwa na ripoti kuwa Waafrika waliokuwa katika jeshi la Kanali Gaddafi wanauwawa, wengi wao wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia Mali na Niger.
Inaarifiwa magari 60 yameingia Niger kutoka Libya, lakini yalizuwiliwa mjini Agadez.
Watu hao wengi ni wapiganaji wa zamani wa kabila la Tuareg, ambao walipatana na serikali ya Niger mwaka 2009.
Inaarifiwa kuwa magari 10 nayo yameingia Mali.
Mapema mwaka huu, wakuu wa Mali waliiambia BBC, kwamba Wa-Tuareg wakilipwa dola elfu 10 kujiunga na serikali ya Libya, na kila siku ya mapigano wakipata dola 1000.
Duru za mataifa ya magharibi zinasema Waafrika kama elfu 10 waliajiriwa na Gaddafi.
Sasa ndege za Nato zinarusha vikaratasi na kutoa matangazo, kuwasihi Waafrika waasi na watapokelewa kufwatana na sheria

Tripoli inahitaji msaada

Uingereza inasema itapeleka chakula na madawa Libya, ambayo yanahitajika sana wakati mapigano yanaendelea katika hatua ya mwisho ya kumuondoa Kanali Gaddafi ambaye amejificha.
Wapiganaji mjini Tripoli
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, anasema upungufu wa vitu muhimu katika mji mkuu, Tripoli, unahatarisha maisha.
Sehemu kubwa ya Tripoli haina maji, mahospitali hayana dawa za kutosha, na chakula na mafuta ni shida kupatikana.
Juma zima hili maji ya bomba katika mji mkuu yamekuwa yakikauka taratibu.
Karibu Tripoli nzima sasa haina maji na sehemu nyingi hakuna umeme.
Baadhi ya maduka yanafunguliwa lakini hayakupata shehena siku kadha.
Petroli na diesel inapungua.
Barabarani kuna mirunda ya taka.
Baadhi ya hospitali zinafanya kazi sawasawa lakini moja, kwenye mtaa wa Abu Salim, ambako mapigano bado yanaendelea, imehamwa na madaktari na wauguzi waliokuwa na hofu.
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limekuta maiti zikiooza za wagonjwa 200 waliokufa.
Serikali inayochukua madaraka ya Baraza la Taifa la Mpito, inadai kuwa sasa inadhibiti asili mia 95 ya mji mkuu, lakini mapigano yanayoendelea na khofu iliyokuwako, inaumiza sana mji.

Friday, 26 August 2011


Ferguson aishambulia FA

Alex
Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson amekituhumu chama cha soka cha England FA kwa kutoipa haki Manchester United.
Meneja huyo wa United, ambaye msimu uliopita alipewa adhabu ya kukaa jukwaani katika mechi tano, ametoa tuhuma hizo wakati akizungumza kuhusiana na wachezaji wake wanane kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England.
Ferguson, 69, alisema: "FA huenda wanafahamu nani ameleta wachezaji zaidi kwa nchi yao kuliko timu yeyote ile duniani.
"Labda watafahamu umuhimu wetu kwa England kuliko kutufanya kama 'takataka'.
Matamshi ya Ferguson yamekuja wakati akizungumzia idadi ya wachezaji wake ambao huenda wakaitwa kuichezea timu ya taifa mwishoni mwa wiki.
Meneja Fabio Capello anatarajiwa kutaja kikosi chake kwa ajili ya michuano ya mwezi ujao ya kufuzu Euro 2012, dhidi ya Bulgaria na Wales. Manchester United huenda ikatoa wachezaji takriban wanane.
Ferguson amefurahishwa na hilo lakini ametumia nafasi hiyo kuishutumu FA kuhusiana na adhabu ilizopewa klabu hiyo msimu uliopita.
"Nafurahia wachezaji wangu, ni wazuri."
FA imegoma kuzungumzia tuhuma za Ferguson.

Adebayor aenda Tottenham

Tottenham imethibitisha kumsajili mshambuliaji Emmanuel Adebayor kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka Manchester City.
Ade
Emmanuel Adebayor
Mapema wiki hii meneja wa Tottenham Harry Redknapp alithiibitisha kuwa klabu yake iko katika mazungumzo na City kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
Adebayor hakuwa kipenzi cha meneja wa Man City, Roberto Mancini mwaka jana, na hivyo kupelekwa Real Madrid kwa mkopo.
Spurs pia wamemsajili kiungo kutoka Uhispania Yago Falque kutoka Juventus ya Italia.
Spurs na City wamekuwa wakizungumza kwa muda kuhusiana na mkataba wa Adebayor, huku ikiripotiwa kuwa mshahara wake wa pauni 170,000 kwa wiki ukiwa ndio kikwazo kikubwa.
Mancini aliweka wazi kwa mshambuliaji huyo kutoka Togo, aliyejiunga na City akitokea Arsenal kuwa hana nafasi kubwa kutokana na kuwepo kwa Carlos Tevez, Sergio Aguero, Mario Balotelli na Edin Dzeko.
Mwezi April Adebayor alisema angependa kusalia Real Madrid.
Adebayor alifunga mabao mawili dhidi ya Tottenham katika robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Bernabeu msimu uliopita.

Watu milioni 12 waishi bila utaifa

Watoto wasio na utaifa
Takriban watu milioni 12 duniani kote hawana uraia wa nchi yeyote, na matokeo yake kunyimwa haki zao za msingi za kibinadamu, umoja wa mataifa umeonya.
Umoja huo unatoa wito wa nchi nyingine kutia saini makubaliano mawili ya kutokuwa na utaifa.
Umesema hali hiyo inazidi kuwa mbaya kwani watoto wasio na utaifa wanazaliwa na wazazi wasio na utaifa.
Tatizo hilo limeenea zaidi kusini mashariki mwa Asia, Asia ya Kati, Mashariki mwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.
Antonio Guterres wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi alisema, "Hawa watu wamekata tamaa na wanahitaji msaada kwasababu wanaishi kama vile wamesahaulika kabisa kisheria."
"Mbali na huzuni inayosababishwa kwao wenyewe, athari ya kubagua makundi ya watu vizazi hadi vizazi inasabisha usumbufu mkubwa katika jamii wanazoishi na mara nyingine ndio chanzo cha migogoro."

Umoja wa Mataifa washambuliwa Nigeria

Kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali nchini Nigeria - Boko Haram - kimedai kuhusika na shambulio dhidi ya makao makuu ya Umoja wa mataifa katika jiji la Abuja.
Msemaji wa kundi hilo alitoa madai hayo alipoongea kwa simu na afisi za BBC nchini Nigeria.
Kikundi hicho kilifanya mashambulio kama hayo dhidi ya makao makuu ya polisi mjini Abuja mwezi Juni mwaka huu.
Mkuu wa polisi wa Abuja Mike Zuokumor aliwaambia waandishi wa habari kwamba mshambuliaji aliyejitoa mhanga alifariki dunia papo hapo kwani mlipuko huo ulimkata vipande vipande.
Umoja wa Mataifa umesema kumekuwa na shambulio la bomu katika jengo la Umoja wa Mataifa nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Abuja
Mlipuko mjini Abuja
Mwandishi wa BBC Bashir Sa'ad Abdullahi ambaye yupo katika eneo la mlipuko amesema ghorofa ya chini ya jengo hilo imeharibika sana.
Huduma za dharura zinaondoa miili ya watu kutoka katika jengo hilo huku majeruhi wengine wakipelekwa hospitali, anasema mwandishi wetu.
Makundi ya wanamgambo wa Kiislam wamekuwa wakifanya mashambulio katika jiji hilo katika siku za hivi karibuni.

Magaidi

Bomu la kutegwa ndani ya gari lililipuka katika kituo cha polisi mwezi Juni na kulaimiwa kundi la Boko Haram, kundi ambalo linataka Nigeria kuanzisha matumizi ya sheria za Kiislam, Sharia.
Kwa mujibu wa walioshuhudia shambulio hilo- gari moja lilivamia eneo la kuingilia la ua wa makao hayo ya umoja wa mataifa likivunja mageti mawili tofauti huku walinzi wakijaribu kulisimamisha.
Walisema dereva wa gari hilo aliliendesha hadi sehemu ya mapokezi kabla ya kulilipua na kusababisha uharibifu mkubwa kila mahali.
Madirisha ya jengo la Umoja wa mataifa yalivunjwa na vipande vya vioo vilitawanyika kila mahali.
Kulikuwa na matone ya damu katika sehemu za kupitia watu na pia katika bustani na wanasema waliona miili ya watu iliotawanyika kila mahali.

Moshi

Shambulio la siku ya Ijumaa limefanyika takriban saa 5 asubuhi saa za Nigeria, katika eneo la kibalozi, katikati ya jiji la Lagos, karibu na ubalozi wa Marekani.
Kulikuwa na mlipuko mkubwa na moshi kutanda ukitoka ndani ya jengo.
"Niliona miili imetapakaa," Michael Ofilaje, mfanyakazi wa Unicef anayefanya kazi katika jengo hilo amesema, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
"Watu wengi wamekufa."
Amesema alihisi kama "mlipuko huo umetokea chini ya jengo na kutikisa jengo zima".
Polisi wamefunga eneo hilo la tukio.
"Tumepeleka polisi wetu na kundi la wataalam wa mabomu. Hatuwezi kusema watu wangapi wamekufa," amesema msemaji wa polisi wa Abuja, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press.

Thursday, 25 August 2011

DUNIA NI WATU, WATUWENYEWE NDIO SISI


Madaktari wa dharura waliitwa katika nyumba moja hapa Uingereza baada ya kuambiwa kuna dharura ya ugonjwa wa moyo, na kukuta mgonjwa mwenyewe ni paka.
pAKA
Sio huyu lakini..
Huduma ya magari ya kubebgea wagonjwa ilipata simu kutoka kwa bwana mmoja na mke wake wakizungumza kwa hofu na majonzi wakisema kiumbe chao chenye umri wa miaka mitano kimepatwa na mshituko wa moyo. Gari la dharura lilipelekwa haraka katika nyumba hiyo, huku madaktari wakidhani ni mtoto mdogo.
Lakini walipofika, walikuta bwana na mke wake huyo wakiwa wamemshkilia paka wao-- ambaye baadaye alikufa.
Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema jinsi walivyoshtushwa na kushangazwa na tukio hilo. "Yaani hatukuamini tulivyokuta ni paka, na sio binaadam"

HOUSE GIRL, ALETA KIZAA ZAA

ANTI Didy habari yako. Nategemea mzima wa afya na hutasita kunisaidia kunipa ushauri unaonifaa. Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili. Tangu nimeolewa miaka sita iliyopita, nimekuwa na msichana wangu wa kazi mmoja ambaye nimempenda sana hasa kwa kuwalea vizuri watoto wangu na kuwa mwepesi wa kazi. Kutokana na kuishi vizuri na ‘housigeli’ huyu, amekuwa kama mtoto wa nyumbani na hata ndugu zangu na wa mume wangu wanampenda sana na wamemzoea kupita kiasi.

Tatizo hili la kuwazoea ndugu wa mume wangu sasa naona linataka kuharibu ndoa yangu kwani huyu msichana ameanza tabia mbaya na amemweleza mkwe wangu kuwa mimi situlii nyumbani na sina muda wa kumshughulikia mume wangu kwani kazi zote anafanya yeye, mimi kazi yangu kusafiri na kushinda kazini. Huyu mama mkwe wangu kusikia hayo, amekuja juu na sasa anamshinikiza mume wangu aniache eti nashindwa kuhudumia nyumba na badala yake amuoe ‘housigeli’. Mume wangu ameshtuka na amenieleza kila kitu hali iliyonikasirisha sana.

Sasa naomba ushauri wako kwani mama mkwe bado yupo kwangu, je, nifanyeje kabla hajaondoka kurudi kwake? Mama Kelvin Tabata, Dar es Salaam. Mama Kelvin pole sana kwani inaonekana huyo mama mkwe wako hajaelimika vya kutosha. Uzuri wa mwanamke haupimwi kwa kazi za nyumbani pekee, bali kuna mambo mengi na mkwe wako anapaswa kutambua kuwa wewe unafanya kazi hivyo huwezi kukaa nyumbani muda wote na ndiyo sababu ukatafuta msaidizi.

Lakini pia ni vyema ukiwa nyumbani ufanye kazi zilizopo ikiwamo kumpikia mumeo na kumhudumia ipasavyo. Usiwe na hasira za haraka kwa msichana wako wa kazi kwani inawezekana aliulizwa kimtego naye akajibu vizuri tu lakini mkweo akawasilisha kwa mumeo vibaya. Nadhani mumeo pia anapaswa amweleze mama yake kwa upole kuwa wewe unafanya kazi na huwezi kufanya kazi zote za nyumbani. Pia amweleze kuwa huyo msichana wa kazi kamwe hawezi kuwa mke wa mtoto wake.

Naamini mtoto wake akimwelimisha na akawa na msimamo, mama mkwe wako ataelewa au hata kama hataelewa, atashindwa kuendelea kusisitiza anachotaka. Ni vyema pia ukakaa na mshichana wako na kumhoji ilikuwaje hata wakazungumza hayo na mkweo na ukiona kama alichokonolewa basi mtahadharishe akae mbali na mama mkwe na asiwe mwepesi kueleza mambo ya ndani ya nyumba kwa mkweo.

Hata hivyo fanya uchunguzi wako kwa siri na ukiona msichana wako anapalilia ili aolewe yeye, basi ni vyema ukatafuta msichana mwingine wa kazi na huyo kumwondoa ili asije kuharibu ndoa yako. Haina haja kugombana na mtu yoyote kwani naamini huyo mkweo ataondoka na nyinyi mtaendelea na maisha yenu. Pia jifunze kuvumilia kwani wakwe wengine uelewa wao ni mdogo